Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Mgazini kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho mkoani Ruvuma
alipofika kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi baada ya serikali kutoa jumla ya
Shilingi Bil. 50 kwa ajili ya ununuzi mahindi kutoka kwa wakulima. (Picha na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Ruvuma
WAZIRI wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda ameagiza utaratibu wa
ununuzi wa mahindi uzingatiwe huku akionyesha kuridhishwa na namna zoezi hilo
linavyoendeleshwa katika mkoa wa Ruvuma ambao wananchi wameonyesha kuridhika.
Hayo ameyasema leo tarehe 22 Septemba 2021 katika Hamashauri ya
Wilaya ya Peramiho, Mbinga na Songea wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya
siku mbili mkoani Ruvuma kujionea namna zoezi hilo linavyoendelea husuani kwenye
mikoa iliyotangazwa awali kuanza kununuliwa kwa zao hilo.
“Watu wana matarajio makubwa kwamba serikali itanunua mahindi
lakini kiasi chenyewe hatukutangaza kununua yote maana lengo la serikali
lilikuwa kuchangamsha soko na malengo makubwa ilikuwa kumsaidia mkulima
mdogo"
"Kwahiyo niliona baada ya ziara ya Mtwara tulikubaliana na
Naibu Waziri kwamba tutawanyike kuangalia hali inavyokwenda mimi nikasema
nije Ruvuma maana ndio inazalisha mahindi kuliko mkoa mwingine wowote.”
Amekaririwa Mhe Mkenda
Amebainisha kuwa walipofika mkoani hapo walisimama kuangalia
zoezi hilo linavyokwenda na matokeo yameonyesha kuwa wananchi wameridhika na
utaratibu uliopo wa ununuzi wa mahindi.
“Kwa kiasi hicho napenda kuipongeza NFRA na kwa sababu
hawakunifahamu mimi ni nani wakati naingia hata mkuu wa kituo hakuniona
nilizungumza na wakulima wanaouza wamesema utaratibu unaenda vizuri"
"Lakini wamesema kuna changamoto ya magunia ambayo NFRA
wameshaifanyia kazi hivyo isitokee kisingizio kuwa mahindi yameshindwa kuuzika
kwa ajili ya hilo,” Amesema Waziri Mkenda
Amesema tayari bei ya NFRA kununua mahindi imeshatangazwa kuwa ni kaisi cha Tsh 500 lakini inaweza kutokea watu wakaacha kuuza kwa kusubiri bei ipande ambapo alieleza haiwezekani kununuliwa yote.
“Mtu mwenye mahindi mengi asafirishe kwenda kuuza kwenye masoko
makubwa ili kuondoa changamoto kwa ambao mahindi yao hayajanunuliwa, ili ziwepo
takwimu za watu ambao mahindi yao wamenunuliwa kwa bei iliyopangwa na
serikali,” Amesema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
amesema wakulima wapo kidogo lakini ni wafanyabiashara zaidi hivyo kama mkoa
wapo pamoja kutoruhusu suala la ununuzi wa mahindi kugeuka sokomoko badala ya
tija ambayo Rais amedhamiria.
“Nilitoa maekezo na nayarudia kituo cha Ruhiko ambacho ndio
makao makuu ya mkoa huu cha NFRA kitumike kama kituo cha kupokelea mahindi
kulingana na uwepo na maghala na manunuzi yasimame"
"Kama mtu anaweza kuleta gari kubwa (Semi Trailler) lenye
tani zaidi ya 30 huyo siyo mkulima ni mfanyabiashara, kama ni mkulima nitataka
kujua shamba alilolimia lipo wapi maana ni mkulima mkubwa na taarifa hizo
ambazo mkuu wa wilaya atakuwa na taarifa za kila mkulima,” Amesema.
Amewataka wakulima waliopo kwenye orodha iliyotolewa apewe
taarifa za shamba lilipo vinginevyo ajiengue ili apeleke mahindi kwenye masoko
makubwa na si kubanana, na wakulima wadogo waachwe ili mazao yao yanunuliwe.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment