METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 7, 2017

MH FESTO MGINA:MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI NI MAJIPU NITAWATUMBUA TUKIANZA KUAJIRI

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mhe Festo Mgina akizungumza na Mwandishi wa habari juu ya maafisa watendaji wa vijiji vyote vya halmashauri ambao si waadilifu katika kufanya kazi walizopewa.


Na Fredy Mgunda,Mufindi

Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa inakabiliwa kuwa na watendaji wa vijiji na kata ambao sio waanilifu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za wananchi katika vijiji kitu kinachosababisha migogoro mingi huko vijijini.

Akizungumza na blog hii mwenyekitii wa halmashauri ya wilaya ya mufindi Festo Mgina alisema kuwa halmashuri inakabiliwa na watendaji wa vijiji ambao wanatumia vibaya pesa za wananchi na ndio sababu inayosababisha kutoitisha mikutano ya hadhara.

“Mimi kama mwenyekiti wahalmashauri hii ni muumini mkubwa wa utawa bora hasa kwa kuzingatia dhana ya uwazi na uwajibikaji kwasasababu nikizangatia dhana hii basi kila kitu kitaenda vizuri tatizo watendaji wangu hawataki kabisa dhana ya uwazi na uwajibikaji yaani watendaji wangu wa vijiji wengi wao ni mizigo tu kwangu” alisema Mgina

Mgina alisema kuwa wamekuwa wakiwawajibisha pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji hao wa vijiji ili kuepuka migogoro kwa wananchi.

“Wananchi wanachanga pesa za maendeleo lakini unakuta mtendaji ametoka alikotoka na kuanza kuzitafuna pesa za wananchi hiyo sio haki jamani niseme ukweli maafisa watendaji wangu wa vijiji si waadilifu na nitatizo kubwa linalosababisha migogoro mingi huko vijijini”alisema Mgina

Aidha Mgina amekiri kuwa na ubungufu wa maafisa watendaji wa kata na vijiji na ndio sababu inayosababisha kukaimisha viongozi wengine wa serikali kushika nafasi za kuwa maafisa za watendaji.

“Saizi tunawatumia waajiliwa wa serikali hasa maafisa kilimo kuwa watendaji wa vijiji kutokana na kuwa uhabari wa wanayakazi wa kada hiyo na labda niseme ukweli nimepiga marufuku waalimu kukaimishwa nafasi hiyo kwa kuwa hata walimu wengi wamekuwa wakisababisha migogoro kutokana n wao kutokujua nini cha kufanya” alisema Mgina

Mgina alisema endapo Rais wa Jamhuri wa muungano Dr John Pombe Magufuli akitoa ruhusa za kuanza kuajili tutajili watendaji wengi na kuwafukuza watendaji wote ambao sio waandilifu kwa kuwa wanaitia doa halmashauri ya Mufindi.

“Waandishi wa habari mkoani Iringa mmekuwa mashaidi kwa kutoa habari mbaya za utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa vijiji na kata sasa njia sahihi ni kufukuza kazi tu maana tumekuwa tukiwaonya mara kwa mara lakini hawabadiliki bora kuwafukuza tu angalia radio Ebony fm,Nuru fm, magazeti,tv na blogs mbalimbali zinatoa habari mbaya za halmashauri ya Mufindi zinazosababishwa na maafisa watendaji” alisema Mgina

Lakini Mgina aliwashukuru shirika la LEAT kwa jitihada zao za kutoa elimu ya utawala bora kitu kilichowasaidia wananchi kuwa na uelewa mkubwa wa kuhoji kwa viongozi wao ambao si waadilifu ndio maana mara kwa mara tumeona viongozi wakifukuzwa katika nafsi zao za kiungozi.

Kwa upande wake afisa habari wa shirika la LEAT Edina Tibaijuka alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasimamia vilivyo watendaji wa vijiji ili kuzitunza Maliasili walizonazo kwa kuwa wao ndio wanajukumu hilo.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com