Mwalimu
Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa
wilayani Nkasi amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika
nyumba ya kulala wageni mjini hapa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema mwalimu huyo alifariki
dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga karibu
na kituo kikuu cha mabasi yanayokwenda mikoani.
Alisema hadi sasa hajafahami chanzo cha mwalimu huyo kujiua kwa sumu ingawa aliacha ujumbe uliosomeka, “Kama
nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu
lakini asilaumiwe, nisilaumiwe chochote juu ya kifo change”.
Inadaiwa
kwamba siku ya tukio mwalimu huyo alifika katika nyumba hiyo ya kulala
wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na baadaye alikabidhi
funguo na kuondoka kwenda kusikojulikana.
Taarifa
zinadai ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa
amelewa akachukua ufunguo kwa mhudumu na kuingia ndani ya chumba
chake kulala.
Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya mtu akikoroma kwa sauti ya juu hali iliyzua hofu.
Mhudumu alilazimika kuomba msaada kwa wapangaji wengine waliokuwamo ndani ya nyumba hiyo na kuvunja mlango.
Baada
ya kuvunjwa kwa mlango mhudumu huyo akiwa na wapangaji hao, walimkuta
mwalimu huyo akiwa anatokwa mapovu hali iliyowalazimu kumkimbiza
hospitalini lakini wakiwa njiani alifariki dunia.
RPC Kyando alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa utabibu, Mwalimu Sanga alikunywa sumu.
0 comments:
Post a Comment