Mhandisi kutoka Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) Elisante Ulomi akimuonesha maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa Machinjio ya Vingunguti Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa mradi
huo jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo ya maendeleo ya
ujenzi wa mradi wa Machinjio ya Vingunguti kutoka kwa Meneja Mawasiliano
wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya (kulia) na kushoto ni
Mhandisi wa mradi huo Elisante Ulomi.
********************************
Na Munir Shemweta, WANMM
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ametembelea mradi wa ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti na kuvutiwa na
kasi ya ujenzi wa mradi huo inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) ambapo alilitaka shirika hilo kuhakikisha linajenga jengo lenye
ubora.
Akiwa
katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana,
Dkt Mabula alisema pamoja na mradi huo kutakiwa kukamilika katika
kipindi cha miezi mitatu badala ya 12 ya awali lakini hatarajii kuona
Shirika la Nyumba linajenga jengo lililo chini ya kiwango.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, NHC ni
shirika la umma lenye kila fani katika masuala ya ujenzi hivyo basi
ujenzi wa mradi huo ujenge imani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na watanzania kwa kukamalisha mradi huo katika kipindi cha
miezi mitatu.
Dkt
Mabula alisema, Maelezo ya Rais kuhusiana na mradi wa machinjio ya
Vingunguti ubadilishe fikra za Shirika la Nyumba la Taifa katika miradi
yake mbalimbali sambamba na kuonesha uwezo katika miradi waliyopewa kwa
kujenga kwa kasi na kwa muda mfupi ukilinganisha na makampuni mengine ya
ujenzi.
‘’Tuondoke
katika fikra tuliyokuwa nayo huko nyuma, tujenge trust kwa mhe Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ alisema Dkt Mabula
Kwa
upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Muungano Saguya alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kuwa shirika hilo limejipanga kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha linakamilisha ujenzi katika muda uliopangwa.
Alisema
ujenzi wa mradi huo wa machinjio ya Vingunguti umefikia hatua nzuri na
ana imani kutokana na jinsi shirika lilivyojipanga katika mradi huo,
ujenzi wake utakamilika katika muda uliopangwa kama ilivyoelekezwa na
rais.
0 comments:
Post a Comment