Luteni
Jenerali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov wa Urusi ndiye mgunduzi wa
silaha maarufu sana katika uwanja wa mapambano duniani kote iitwayo AK
47. Ni bunduki iliyobuniwa na kutengenezwa na kamanda huyu wa Jeshi
Jekundu (Red Army) la Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) wakati huo.
Luteni
Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alizaliwa tarehe 10 Novemba
1919 eneo la Kurya, Altai, Urusi, ambalo kwa sasa linajulikana kama
Altai Krai, Russia. Alijiunga na jeshi la Urusi mwaka 1938 na kupangiwa
kama fundi wa vifaru na baadaye alipanda cheo na kuwa kamanda wa vifaru.
Mwezi
Oktoba mwaka 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alijeruhiwa vibaya
katika mapigano ya Bryansk na kulazwa hospitalini mpaka mwezi Aprili
mwaka 1942. Akiwa hospitalini akitibiwa, aliwasikia askari wenzake wa
Kirusi wakilalamikia udhaifu wa bunduki zao za Urusi katika uwanja wa
mapambano.
Baada
ya kubaini udhaifu huo wa bunduki za Urusi, aliamua kutumia ubunifu
wake kutengeneza bunduki bora zaidi za jeshi la nchi yake. Baada ya
majaribio yake ya muda mrefu, hatimaye juhudi zake zilizaa matunda mwaka
1947 alipofanikiwa kutengeneza bunduki ya AK 47. Jina hili AK 47 ni
kifupi cha maneno "Avtomat Kalashnikova model 1947"; namba 47 inasimama badala ya mwaka wa ugunduzi.
Luteni
Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alifariki hospitalini tarehe
23 Desemba, 2013 akiwa na umri wa miaka 94 huko Izhevsk, mji mkuu wa
jimbo la Udmurtia Urusi.
Huyo ndiye MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV, mgunduzi wa bunduki maarufu kwa jina la AK 47 ["Avtomat Kalashnikova model 1947"].
0 comments:
Post a Comment