METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 16, 2017

ELIBARIKI KINGU:NILIMSINGIZIA MAKONDA BILA KUJUA

Mbunge wa Singida Magharibi kupitia CCM mheshimiwa Elibariki Kingu amesema alipotoshwa kuhusu tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda .Kingu ameyasema hayo leo baada ya kukutana na mkuu huyo wa mkoa na kumweleza nia yake ya kumuomba radhi juu ya yale yote aliyoshiriki kwa namna moja ama nyingine kumchafua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Miezi kadhaa iliyopita mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda aliingia kwenye vita kali na makundi mbalimbali ya kijamii wengi wao wakiwa wanasiasa na wafanya Biashara kwa kile ambacho kilidaiwa vita dhidi ya madawa ya kulevya na tukio linaloitwa uvamizi kwenye kituo cha luninga cha Clouds.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mbunge huyo amesema amejutia kitendo chake cha kumtuhumu Makonda bila kuwa na taarifa sahihi na kusisitiza kuwa ni wakati sasa wananchi hususani vijana kuacha kusingiziana mambo ambayo hatuna uhakika nayo pia amewataka wananchi kutoongozwa na chuki binafsi dhidi ya viongozi wao.Huyu kijana Makonda ana kipaji sana na siku ya leo nimepata ukweli juu yake kuhusu kusingiziwa kwa magari na madudu mengi,moyo wangu uliumia sana na nikamwomba Mungu anipe kuusafisha moyo wangu na kunisamehe maana hakika niliaminishwa uongo amesema mbunge huyo.Mungu akulinde kaka,Hakika Mungu wetu sio mwongo,Bwana wa utukufu akutunze Rc Makonda,alimaliza kwa kusema Elibariki Kingu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa amesema hana kinyongo na mtu yoyote akiwemo mbunge huyo kwani yaliyomkuta wakati akiendesha vita dhidi ya madawa ya kulevya ni mambo ambayo hata kabla ya kuingia kwenye vita hiyo alijua yatatoke kwa sababu ya ugumu wa vita hiyo.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com