METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 16, 2017

IJUMAA KAREEM KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. PAUL MAKONDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, *Mhe Paul Makonda* amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikitini zaidi ya *Mia sita (600)* ya Mkoa wa Dar es salaam.

Hatua hii ni muendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, ambapo katika kuenzi mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.

*Mhe Makonda* ametoa vitu mbalimbali kama *SADAKA KWA KILA KIONGOZI* vifuatavyo kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam :-
*1. Mchele Kg 25*
*2. Ngano Kg 25*
*3. Sukari Kg 25*
*4. Mafuta ya kupikia Lita 20.*

Akizungumza na Masheikh na  Viongozi wa Dini ya *KIISLAMU,* Mhe Makonda kwanza amewapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe, Rais, *Dkt. John Pombe Magufuli* kwa jinsi ambavyo anatekeleza utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye nchi ya Uchumi na kipato cha kati kupitia mapinduzi ya *VIWANDA.*

*Mhe Makonda* pia, amewaomba viongozi wa Dini kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuhubiri *AMANI, UTULIVU NA KUVUMILIANA* katika kila mambo wanayofanya waumini wao.

Katika hatua nyingi, *Mhe Makonda* amefanikiwa *KUWASHAWISHI* wafanyabiashara haswa wa *SUPERMARKET* Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha *mfungo wa Ramadhani.*

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu* *wa Mkoa wa Dar es salaam*
*Kitengo cha Mawasiliano.*
*16/06/2017*

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com