METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 12, 2017

DC SENYAMULE AWASIHI WAJASIRIAMALI KUTOOGOPA KUKOPA

Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza wakati wa Mkutano na Wajasiriamali Uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo uliopo katika Kata ya Same Mjini
Picha ya pamoja Kati ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Same na Wajasiriamali waliojitokeza kwenye Mkutano wa Wajasiriamali
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi Anna-Claire Shija akizungumza wakati wa Mkutano na Wajasiriamali Uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo uliopo katika Kata ya Same Mjini
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Same Ndg Augustino Kessy akitoa neno kwa wajasiriamali hao wakati wa Mkutano
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Sitini wakati wa Mkutano na Wajasiriamali Uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo uliopo katika Kata ya Same Mjini

Na Paschalia George, Kilimanjaro

Wajasiriamali wametakiwa kutoogopa kukopa kwani kutegemea mtaji mdogo pekee haiwezi kuwa sehemu rahisi katika mafanikio.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule Wakati akizungumza kwenye Mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata ya Same Mjini.

Mhe Senyamule amesema kuwa ili kufanikiwa zaidi wajasiriamali hao wanapaswa kukopa kwa  malengo ya kuendelea kuzalisha na sio kununulia Vitu kwa ajili ya kufanyia starehe kwani kufanya starehe kutarudisha nyuma mzunguko Wa pesa.

Katika Mkutano huo Mhe Senyamule amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 60 kwa vikundi 29 vya wajasiriamali wadogo wadogo Wa Same ambapo amesema kuwa fedha hizo ni za mikopo hivyo ninapaswa kurudishwa kwa utaratibu uliowekwa ili na wengine wapate kwa wakati na kufanya zoezi kuwa endelevu.

Aidha amewataka wajasiriamali hao kufanya kazi kwa bidii na kuepuka kero ya kufunguliwa kesi pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo hiyo.

"Serikali ya sasa inataka watumishi na wananchi tuwe wachapa kazi na waadilifu hivyo basi mikopo hii itumike kwa uadilifu kama ilivyokusudiwa" Alisema Mhe Staki

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi Anna-Claire Shija alisema kuwa wajasiriamali ni watu muhimu kwa kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi, kupunguza umasikini miongoni mwa watu hivyo Kama mikopo hiyo ikitumiwa vizuri itanufaisha vizazi vya watanzania wote.

Bi Shija alisema kuwa ujasiamali hutoa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuli mpya lakini pia ni ujira binasfsi na nafasi za ajira kwa watu wengi hupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu sambamba na 
hupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com