METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 17, 2017

CCM YAKUBALIKA KWA WANANCHI KWA ASILIMIA 65%

Kalamu ya Beatrice Condrad
Kutoka Kwa ndg Humphrey Polepole

Siasa si kupiga domo, siasa ni kutoa uongozi safi tena safi kabisa si kupiga domo hata kidogo ndo maana mimi sisemi semi sana tunasimamia utekelezaji wa SERA sasa ivi, siasa si kupiga domo hii kupiga domo ndo iliyotufikisha hapa pahala tumeharibikiwa kwa sasa SIASA maana yake ni: kuangalia Sayansi ya matokeo ya Utafiti kama haya kisha kuya actualize  kwenye maisha ya watu. Sasa hawa waliosema wamezuiliwa kuongea hawa ni waongo na wanafiki kabisa Mimi nimekuwa kiongozi wa serikali kabla sijaanza kufanya Kazi kwenye Chama Cha Mapinduzi nilikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo hapa Dar Es Salaam

Ubungo kuna majimbo mawili KIBAMBA na UBUNGO hawakutaka kwenda kufanya maandamano nilikuwa pale kama kiongozi wa Serikali WANANCHI wa pale walikuwa wakilalamika kulingana na kiongozi walio wachagua kutokurudi kuwasikiliza shida zao WANANCHI wa pale walikasirika sana Kwa aina ya uongozi waliouchagua pale, munaposema mumezuiliwa tafsiri yake nini? Arusha pale wapo opposition hawaandamani kila siku siku ,Moshi IPO opposition andamaneni andamaneni Mbeya mjini pana opposition andamaneni ndugu zangu msifanye Kazi hawahandamani

Wanangangania watu waandanane kwenye maeneo ambayo Chama Cha Mapinduzi kinatekeleza ipasavyo ilani ya Ccm  lengo lao nikuwapotezea WANANCHI wetu kuwapotezea muda ili ikifika mwisho wa siku serikali ya chama cha Mapinduzi kutupiwa lawama, uzuri wa wananchi wetu wameshaelewa nia mbaya iliyopo kwenye hivi vyama vya upinzani wamekaa kuilaumu serikali badala ya kushirikiana na WANANCHI wake kutatua kero zao, Chama cha Mapinduzi  kinatoa maendeleo Kwa watu wake tunafanya Kazi Kwa bidii kwenye falsafa ya ( HAPA KAZI TU) wanawang'ang'aniza WANANCHI wasifanye Kazi this is not fair haiwezekani, Wanasiasa Uchwara uchwara WANANCHI ni vizuri wakawatazama Kwa jicho la pili

Kwanini hawaandamani Kilimanjaro Moshi nilikuwa huko juzi Kwa maswala yangu ya kisiasa kule mambo yapo vizuri WANANCHI wameshaielewa serikali ya Chama cha Mapinduzi kuwa ina dhamira ya dhati kabisa Kwa WANANCHI wake Kyle siku hizi hawaandamani wameshaelewa kuwa wanaotaka waandamane familia zao wanazisafirisha nje ya nchi huku watoto wa familia za kawaida kuumia, kule Kigoma ujiji huyu Bwana Zitto ana jumbo moja nchi nzima na kiongozi wao mkubwa anatoka pale hawaandamani ningependa kuona maeneo yao wanaandamana Mara dufu kisha waseme sehemu nyingine hatuandamani  haiwezekani na katika siku zinavyokwenda chama cha Mapinduzi kinazidi kushughulikia Keri za WANANCHI wake ndo maana kadiri siku zinavyokwenda chama cha Mapinduzi kinazidi Kukubalika

Ukichukua chama cha Upinzani cha Tundu Lissu, ukichukua chama cha Upinzani cha Zitto Kabwe ukichukua Chama cha Upinzani cha ndugu Mbatia Ukichukua chama cha Upinzani cha Mzee Lipumba Kwa pamoja ukivijumlisha Chama cha Mapinduzi Kinakubalika na WANANCHI zaidi ya asilimia 65% sasa Kwa TAKWIMU hizi tusipotoshe watu wetu ,mutuache sisi tutor maendeleo Kwa watu na sisi tumeshajipanga kupata asilimia zaidi ya 70% mwaka 2019 kwenye chaguzi za serikali za mitaa and your so determined

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com