METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 26, 2017

WAFUASI WA ODINGA WAINGIA BARABARANI

Image result for nasa coalition demonstration

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya ‘IEBC’, Ezra Chiloba ametangaza kuachia ngazi leo huku wafuasi wa Muungano wa Upinzani (NASA) wakifanya maandamano katika baadhi ya maeneo nchini humo kushinikiza kuondolewa kwa maafisa 12 wa tume hiyo akiwemo Ofisa huyo kwa shutuma za kuvuruga uchaguzi wa Agosti 8, mwaka huu.

Maandamano hayo yaliyotawaliwa na ghasia katika baadhi ya maeneo ni mwitikio wa wito uliotolewa jana na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga aliyewataka wafuasi wake kujitokza kwa wingi kuandamana hadi Makao Makuu ya IEBC, ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Mahakama ya Juu Kenya kufutilia mbali matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.

Wafuasi wa NASA walikuwa wakimshutumu Chiloba na watendaji wengine kufanya njama za kuingilia mchakato wa uchaguzi huo na kumsaidia Rais Kenyatta kuibuka kidedea.

Waandamanaji hao wamebeba matawi ya miti, mabango, huku wakipiga mayowe na honi za pikipiki kuanzia barabara ya Obote, kisha mtaa wa Oginga Odinga kabla ya kuchukua barabara kuu ya Kenyatta hadi Mtaa wa Ang’awa katikati ya Jiji la Nairobi huku watu wachache wakiwa wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.


Haya yanajiri ikiwa ni siku 30 tu zimesalia hadi kufanyika uchaguzi wa marudio, Oktoba 26, mwaka huu
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com