Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma
Zuberi Homera, leo 16/06/2017 amehudhuria sherehe ya siku ya mtoto wa afrika kiwilaya iliyofanyika Tunduru mjini.
DC Homera aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Tunduru, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mhe. Mbwana Mkwanda Sudi, wakuu wa Idara mbali mbali wa halmashauri ya Tunduru na watendaji wa vijijj na kata ya Nanjoka Tarafa ya Mlingoti.
Historia ya siku ya mtoto wa afrika ni mauwaji ya watoto huko afrika kusini katika kutongoji cha soweto, watoto hao waliuwawa wakidai haki zao tarehe 16/06/1976. kwa kuwa ilionekana hakuna chombo chochote cha kutetea haki za watoto hivyo mwaka 1987 mkataba wa haki za watoto ulipitishwa na umoja wa mataifa ambapo umoja wa nchi huru za afrika uliazimia kuenzi siku hii, Tanzania iliridhia kutia saini mkataba huo mwaka 1991.
Sherehe hii maalum iliwakutanisha wanafunzi pamoja na walimu wao kutoka shule mbali mbali wilayani Tunduru.
Shughuli hio ilianza kwa igizo maalum toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tunduru mchanganyiko na baadae Bunge la wanafunzi lililokuwa na mjadala wa kutetea haki za watoto kama vile haki ya kutonyanyaswa, haki ya kusikizwa, haki ya kutobaguliwa na haki ya kupata Elimu.
Akizungumza kwenye sherehe hio Mkuu wa wilaya ya Tunduru alieleza hisia zake za dhati za kutaka watoto wote waende shuleni kwa kuwa hakuna sababu ya mtoto yeyote nchi hii kutokwenda shule kwa sababu serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefuta Ada na miundombinu ni rafiki kwa kila mtoto na hata mtoto mlemavu anapaswa kwenda shuleni.
"Tunayo shule ya msingi Tunduru mchanganyiko ambayo inapokea wanafunzi walemavu, serikalini kuna viongozi mbalimbali ambao ni walemavu wamefika walipo kutokana na kuzingatia masomo".
Kuhusu suala la fursa sawa Dc Homera alieleza kwamba serikali tayari imeleta vifaa vya kujifunzia katika masomo kwa walemavu na vipo vinavyotumika shule ya msingi Tunduru mchanganyiko.
Alisisitiza wananchi waache tabia ya kufanya sherehe mtoto akimaliza Darasa la saba.
"Ni marufuku kufanya sherehe za kumaliza Darasa la saba, tusubirie hadi kidato cha nne angalau tuanze kufanya sherehe".
Akizungumzia haki za watoto DC Homera alisema, kumekuwa na tabia zikihusisha baadhi ya wazazi kuwa nyanyasa watoto mfano kuwabaka, katika kijiji cha Semeni tuliwaweka ndani viongozi na wazazi kwa sababu ya kuwa nyanyasa watoto na kuna baadhi ya watumishi sio waaminifu.
"Mfano mtoto kabakwa wao wanajaribu kufuta ushahidi, hivyo nawaomba matukio hayo myalete ofisini kwangu".
Akizungumzia tatizo la watoto kufanyishwa kazi kupita kiasi DC Homera alisema watoto hawapaswi kupewa kazi kupita kiasi.
"Mtoto anapaswa kufanya kazi Kidogo na ikifika saa moja na nusu watoto wote waruhusiwe kwenda kujisomea".
Akitoa maelezo kwenye swala la watoto wa kiume kupelekwa jando alisisitiza wazazi wasubirie shule zifungwe sio mtoto anakatizwa masomo kisa jando za asili.
Dc Homera alisisitiza wazazi lazima waalikwe kwenye sikukuu ya mtoto wa Africa kwani wao pia ni wadau muhimu katika kutekeleza haki za watoto.
Akaongeza kwamba Swala la Afya ni haki ya Kila mtoto kuwa na Afya njema na sasa hivi ujenzi wa kituo cha Afya nakayaya tumeanza ujenzi wa jengo la utawala na mengine unatafuata kama vile maabara, chumba cha upasuaji na wodi.
Wakati huo huo, Mhe. Homera anatarajia kujenga madarasa kumi na moja hasa katika shule zenye mazingira magumu zaidi na chanzo cha pesa ni mchango ya Wadau mbalimbali pamoja na wizara hisika na kama serikali ya wilaya tutaanzisha mfuko maalum wa Elimu wa wilaya kupitia zao letu la korosho.
Aidha, DC Homera aliwaomba wazazi pamoja na jamii tushirikiane kulinda haki 10 za watoto na wazazi wahakikishe wanawafungulia watoto wao akaunti ya benki na Kila mwezi angalau waweke elfu ishirini, kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mtoto wa afrika ni "MAENDELEO ENDELEVU 2030: IMARISHA ULINZI NA FURSA SAWA KWA WATOTO".
0 comments:
Post a Comment