Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imeanza kutekeleza Waraka No.3 wa Mwaka 2014 kuhusu posho ya madaraka toka Julai 2016.
Hayo yameelezwa Leo tarehe 19 Mei, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi Seleman Jafo alipokuwa akijibu swali la msingi la Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza kulipa posho hizo.
Kufuatia majibu Hayo, Chumi aliuliza kuwa, kwa kuwa posho hiyo ni ya madaraka je ni lini Serikali itaanza kuwalipa posho ya madaraka viongozi wengine kama Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma na Afisa Elimu Takwimu na Vielelezo.
Akijibu swali Hilo, Jafo alisema kuwa kwa kuwa vyeo hivyo ni vya muundo, Serikali itaangalia kulingana na tathimini inayofanywa na Utumishi.
Aidha, Mbunge huyo wa Mafinga alihoji ni lini serikali itaanza kulipa posho ya kufundishia kwa waalimu wote.
"Kazi ya ualimu ni zaidi ya kufundisha, Kuna kufanya maandalio, kufundisha, kusahisha, kupanga matokeo na majukumu mengine mengi, je serikali iko tayari Sasa kulipa teaching allowance kama ilivyokuwa siku za nyuma ' Aliuliza Chumi.
Mbunge wa Buyungu ambaye ni mwalimu kitaaluma Kasuku Bilago alihoji zaidi kwamba ni makosa kulinganisha kada ya ualimu na Kazi nyingine,
Mwalimu anaendelea na Kazi hata anapokuwa nyumbani, sio Sawa na Afisa kilimo, hivyo ni muhimu kuzingatia kuwalipa teaching allowance.
Katika majibu ya swali la msingi la Chumi, Naibu Waziri wa Tamisemi alizitaja posho hizo za madaraka zinazolipwa kwa kuwa ni Tsh. 200,000/= kwa Waalimu Wakuu, Tsh. 250,000/= kwa Wakuu wa Shule na Waratibu wa Elimu na kwamba Kati ya Julai 2016 hadi April 2017 Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 1.87 kwa ajiri ya kuimarisha usimamizi wa Elimu Katika ngazi ya Shule nchini.
Posho hizo za madaraka na teaching allowance imekuwa kilio cha wadau wengi wa Elimu.
Katika Bunge la Bajeti la 2016 wabunge walihoji kwanini Serikali imekuwa haitekelezi Waraka huo ambao ulitolewa toka 2014.
0 comments:
Post a Comment