
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo
akiongea wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii lilofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo
pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii
wakiimba wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii lilofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo
akikabidhiwa zawadi na Rais wa Chama cha Maafisa Maendeleo ya Jamii
CODEPATA Bw. Wambura Sunday huku viongozi wengine wa Wizara yenye
dhamana na Maendeleo ya Jamii wakishuhudia mara baada ya kufunga
kongamano la wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo
pamoja na mke wake amabye pia ni Afisa Maendeeo ya Jmaii mkoa wa Dodoma
wakifurahia zawadi iliyotolewa na wataalam wa maendeleo ya jamii mara
baada ya waziri huyo kufunga kongamano lao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na
Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wataalam wa
Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*******************************
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jafo
ametao mwezi mmoja kwa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinafungua
akaunti maalum ya Benki kwa ajili ya fedha za maendeleo ya vijana,
wanawake na watu wenye ulemavu.
Waziri Jafo
ametoa agizo hilo jana wakati akifunga kongamano la wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma nakuwataka wataalam hao kuhakikisha
wanakwenda kusimamia zoezi hilo na kukamilisha katika kwa kipindi cha
mwezi mmoja.
‘’Natoa maagizo
ifikapo Novemba, 30 kila Halmashauri Nchini iwe imefungua akaunti maalum
ya Benki kwa ajili fedha ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa
kuwa fedha zikitolewa katika mfumo wa sasa zinakuwa kama zinaelea’’.
Alisitsiiza Waziri Jaffo.
Aidha Waziri Jafo
aliongeza kuwa fedha hizi zinapotelewa bila akaunti hiyo inakuwa vigumu
kwa serikali kuzifanyia tathimini hivyo kuwaimiza wataalam wa sekta ya
maendeleo ya jamii katika Halmashauri zao kuhakikisha wanatekeleza agizo
hilo ili malengo na matumizi ya fedha hizo yaweze kufanyiwa tathimini.
Pamoja na kutoa
agizo hilo Waziri Jafo pia ameongeza kuwa ili jamii iweze kuleta
mabadiliko yanayotakiwa suala la kutumia wataalam wa maendeleo ya jamii
halikwepiki kwa sasa wakati jamii inataka mabadiliko ya haraka kuelekea
Tanzania ya viwanda.
Wataalam hawa ni
chachu ya mabadiliko na katika mashirika makubwa duniani wataalam wa
maendeleo ya jamii wamekuwa wakitumiwa sana ili kuleta mabadiliko katika
nyanja mbalimbali na wamekuwa msaada mkubwa kitaifa na kimataifa.
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika
hotuba yake kwa Waziri huyo aliongeza kuwa kongomano hilo lilikuwa na
mjadala mkubwa kuhusu kuhamasisha jamii kujiletea maendeleo kwa kutumia
istilahi zilizoko katika jamii akitolea mfano wa istilahi maalufu kwa
mikoa ya ya kati ijulikanayo kama Msalagambo.
Aidha Dkt. Jingu
aliongeza kuwa matokeo ya kongamano hilo pia nikuwafanya wataalam hao
wajione kuwa wao ni chachu ya maendeleo katika kuhamasisha wananchi kuwa
na ari ya kujiletea maendeleo.
Wakati huo
huo Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka TAMISEMI aliyemwakilisha Katibu
Mkuu wa Wizara yake katika Kongomano hilo Bw.John Miayo Cheo aliwataka
wataam wa maendeleo ya jamii kutumia taaluma yao kuhamasisha wananchi
kugombea nafasi za uongozi ili waweze kuwa viongozi wa kufuatia uchaguzi
ujao wa Serikali za Mitaa.
Wataalamu wa
Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamekutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu
wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata
maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo
wa siku nne
0 comments:
Post a Comment