Miradi mbalimbali ya Uwekezaji inayotaraji kufanyika ndani ya Jimbo la Ilemela itakuwa fursa ya kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.
Hayo yamebainishwa na balozi mstaafu wa Korea katika mazungumzo yake na viongozi wa Ilemela akiwemo Mkuu wa wilaya Ilemela Mhe Dkt Leonard Masale, Meya wa Manispaa Ilemela Mhe Renatus Mulunga, Naibu Meya Mhe Shaban Maganga, Kaimu Mkurugenzi Mhe Daniel Batare, Katibu Ofisi ya Mbunge Heri James, wataalamu wa Manispaa Ilemela na wageni alioambata nao kutoka nchini Korea.
Aidha Ugeni huo wa uwekezaji ulianza kwa kufanya kikao kifupi na mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela na baadae kutembelea maeneo yaliyotengwa kwa utekelezaji wa miradi yakiwemo Ihalalo, Nyamhongolo, eneo la mafunzo ya kilimo chini usimamizi wa The Angeline Foundation Imalang'ombe na shule ya sekondari wavulana Bwiru.
Balozi huyo mstaafu wa Korea Kim Young Hoon amesema kuwa anafurahishwa na kasi ya maendeleo ya Jimbo la Ilemela na kuongeza ni matumaini yake kuona miradi ya uwekezaji itayotekelezwa ikileta manufaa ya kukua kwa uchumi wa pande zote mbili .
'Nafurahishwa na kasi ya ukuaji wa mji wa Ilemela sambamba na ushirikiano kutoka wa muasisi wa mahusiano ya pande hizi mbili chini ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula , Matumaini yangu kuona uwekezaji tunaoufanya ukichochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi wetu' Alisema .
Nae mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Dkt Masale na Meya wa manispaa hiyo Mhe Mulunga mbali na kushukuru kwa maamuzi yao ya kuichagua Ilemela kama eneo la uwekezaji wamemuhakikishia ushirikiano wa utekelezaji wa makubaliano yote katika kufanikisha utekelazi wa miradi hiyo huku wakihimiza mawasiliano ya Mara kwa mara.
Akihitimisha Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Ndugu Heri James amesema Mengi mmezungumza na Dkt Mabula Sisi kazi yetu ni kusisitiza na tunawahakikishia utayari na umakini katika kufanikisha dhamira ya uwekezaji na tunaamini bado tuna mengi yakufanya kwa pamoja.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
07.04.2017
0 comments:
Post a Comment