METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, April 9, 2017

MAKAMU WA RAIS KATIKA HAFLA YA TUZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  jana tarehe 08 Agosti 2017 amewataka wafanyabiashara na wawekezaji Nchini kuongeza kasi mara dufu katika uzalishaji ili Taifa lifikie lengo yaani kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais amesema kwamba Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.

Mhe. Makamu wa Rais amesema mwaka wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi.

Mhe. Makamu wa Rais amesema Serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika *kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati.

Makamu wa Rais wa Nchi yangu mzalendo na mchapakazi.

Nchi yangu...
Matokeo chanyA+

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com