Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na waalikwa katika
hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani
Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli
kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo (katikati) akionesha siaha alizokabidhiwa na Wazee wa Busega kama ishara ya ushujaa kwake wakati wa hafla iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na Mkewe wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, akizungumza na viongozi na waalikwa mbalimbali kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega , katika hafla ya kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo, akimtambulisha Mke wake kwa viongozi na waalikwa mbalimbali kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega , katika hafla ya kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na Mkewe wakizungumza jambo wakati wa hafla ya kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Meatu,Mhe.Joseph Chilongani, Mkuu wa Wilaya ya Maswa. Dkt.Seif Shekalaghe, Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe. Benson Kilangi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Mhe.Festo Kiswaga wakifuatilia jambo wakati wa hafla ya kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuzungumza na hadharailiyoshiriki hafla ya kumpongeza Jenerali Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Buyegu kutoka Jijini Mwanza katika hafla ya kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega
Jaji Msaafu Thomas Mihayo akiwa na Mke wake wakizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo kuzungumza na hadhara iliyoshiriki hafla ya kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega
Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Buyegu kutoka Jijini Mwanza wakitoa Burudani kwa kucheza na nyoa aina ya chatu katika hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli ambayo imefanyika kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa nne kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa mkoa, madhehebu ya dini na katika hafla
ya kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa ambayo imefanyika
kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Uongozi mkoani Simiyu umeomba kuwepo kwa kikundi cha
ulinzi cha kijeshi katika Wilaya ya Busega ili kusaidia mapambano dhidi ya
vitendo vya uhalifu ikiwemo uvuvi haramu na kuwezesha ufugaji wa samaki ndani
ya Ziwa Victoria kufanyika kwa usalama.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo iliyoandaliwa na ndugu zake
kijijini kwao Yitimwila ‘A’ katika Kata ya Kiloleri Wilayani Busega.
“Tumepata changamoto nyingi sana kwenye ziwa,
matukio mengi ya kihalifu liliwemo la uvuvi haramu , sisi kama mkoa tulikuja na
wazo kwamba tungehitaji tupate ‘detouch’ moja eneo la Ziwa ili ukanda huu baada
ya kufanya kazi kubwa ya kuchoma makokoro ya wananchi, tuwapeleke kwenye uvuvi
wa kisasa hususani ufugaji wa samaki ziwani, jambo ambalo Mheshimiwa Rais analipa kipaumbele
sana; na namna pekee ya kufanya ufugaji
ule wa samaki ziwani, suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana; ” alisema
Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema pamoja na
kufanya ufugaji wa samaki katika Ziwa
Victoria, Serikali ya Mkoa imefanya makubaliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
NSSF kuwawezesha wananchi wa Busega kufanya kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia
maji ya ziwa hilo ambayo ni ya uhakika.
“Tumeongea na NSSF kwa ajili ya
kuanzisha mradi ambao hautazidi bilioni
moja, tutaleta mbegu za aina ya nyanya na pilipili zinazotakiwa ili wananchi wa
Busega wazalishe kwa wingi.
Hatutakuwa tayari kuona wananchi wanalima nyanya na kuuza ndoo moja shilingi 500, tumepanga kuanzisha mradi wa kuzalisha ‘chill sauce’ na
‘tomato source’ .”alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa Wataalam wa Wilaya
na Mkoa kwa kushirikiana na Wataalam wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji , Kituo
cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru wanafanya upembuzi yakinifu kuona namna
miundombinu ya umwagiliaji itakavyojengwa ili kuwawezesha wananchi wa Busega
kulima muda wote kupitia kilimo cha Umwagiliaji badala ya kutegemea mvua.
Mtaka amesema Serikali mkoani
Simiyu imedhamiria kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Mkoa
hauingizi bidhaa kutoka mikoa mingine na badala yake wananchi wake watazalisha
na kutumia bidhaa zao wenyewe, hivyo ameomba Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuona
namna ya kuweka vituo vya kuuza zana za kilimo katika maeneo ya kanda ya Ziwa
ili wananchi wapate zana bora za kisasa zitakazowasaidia kulima kisasa.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo amewataka wananchi wa Busega
kubadili mtazamo wao na kutumia maji ya ziwa Victoria kwa manufaa yao kwa ajili
ya kilimo cha umwagiliaji ili wasikumbwe na tatizo la upungufu wa chakula
kunapotokea ukame.
Kuhusu suala la ulinzi katika
Ziwa Victoria amesema ombi la Serikali
ya Mkoa la kuwa na kikundi cha Ulinzi,
viongozi watalitafakari kuona namna ya kulishughulikia na akaeleza kuwa
tayari Jeshi limeweka kikundi kidogo cha kiulinzi kutoka Jeshi la
wanamaji, lakini kutokana na ukubwa wa
Ziwa Victoria kikundi hicho hakiwezi kuhimili kufanya doria maeneo yote na
akaahidi kukiimarisha zaidi.
Jenerali Mabeyo pia amewaasa
vijana wa Busega na mkoa wa Simiyu kwa ujumla kujiunga katika vikundi ili
Serikali iwasaidie kutafuta mitaji ya kujishughulisha na Kilimo, uvuvi na
ufugaji badala ya kukimbilia JKT tu,
japo amesema kwenda kwao JKT kunaweza kuwasaidia kupata stadi mbalimbali
za maisha.
Naye Mwakilishi wa Baraza la
Wazee wa Wilaya ya Busega, Bibi. Perazia Ndaki akisoma risala ya wazee kwa Mkuu
wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amemuomba Mkuu huyo wa majeshi
kuona uwezekano wa kuanzisha Kambi ya jeshi la Kujenga Taifa(JKT) katika mikoa
ya kanda ya Ziwa na hususani Mkoa wa Simiyu ili kuwasaidia vijana wengi kujiunga
na kupata stadi mbalimbali zitakazowasaidia kujiajiri katika uvuvi, kilimo na
ufugaji.
Mbunge wa Jimbo la Busega,
Mhe.Raphael Chegeni amemuhakikishia Mkuu huyo wa majeshi kuwa endapo ombi la
kuanzisha kambi katika Mkoa wa Simiyu litaridhiwa, Wilaya ya Busega itatoa eneo
kwa ajili ya ujenzi wa kambi hiyo ambalo lipo tayari.
Sanjali na hilo viongozi
mbalimbali wa dini walioshiriki katika hafla ya kumpongeza Mkuu huyo wa Majeshi,
wamesisitiza wananchi kuwaombea yeye pamoja na viongozi wote wa Serikali wa ngazi
zote ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwatumikia wananchi.
Hafla ya kumpongeza Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo imefanyika kwa
ajili ya ndugu zake kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika nafasi hiyo, ambapo ilitanguliwa na ibada ya shukrani iliyofanyika
katika Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya Wilayani Busega, Jimbo la Shinyanga.
Imehaririwa na Mathias Canal, www.wazo-huru.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment