Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kikao kikao chao cha kanda kilichofanyika Mjini Bariadi
Mwenyekiti aliyeongoza kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii Kanda ya Ziwa ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya Serengeti, Ndg.Wambura Sunday akizungumza na maafisa hao (hawapo pichani) katika kikao cha kanda Mjini Bariadi
Baadhi
ya Maafisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa
wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(hayupo pichani)
katika kikao kikao chao cha kanda kilichofanyika Mjini Bariadi
Na Stella Kalinga
Maafisa
Maendeleo ya Jamii wametakiwa kutumia taaluma yao kuleta mabadiliko katika
jamii kwa kubaini fursa mbalimbali zinazoweza kuwaletea wananchi maendeleo
katika maeneo yao.
Wito huo
umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini katika ufunguzi
wa Kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Kanda
ya Ziwa kilichofanyika Mjini Bariadi.
Sagini amesema kutokana
na taaluma yao Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaweza kuwasiliana na jamii na
kueleweka kwa urahisi zaidi hivyo watumie fursa hiyo kuwashauri wananchi na
vikundi mbalimbali kufanya shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato ili
waondokane na umaskini.
Amesema wananchi
wengi wanafanya shughuli mbalimbali lakini wanakosa elimu, uwezeshwaji na
taarifa sahihi za masoko na mitaji ili
kuendeleza shughuli wanazofanya, hivyo akawataka kutimiza wajibu wao katika
kuelimisha na kuihamasisha jamii kuunda vikundi hususani vijana na wanawake ili watambuliwe na
kuwezeshwa.
Akizungumzia
namna Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Simiyu walivyoshiriki katika
maendeleo ya Simiyu ya Viwanda, amesema walibaini vikundi vya vijana katika
maeneo yao na kubuni uanzishwaji wa viwanda vidogo wiwili ambavyo ni Kiwanda
cha kutengeneza Chaki (Maswa) na Kiwanda cha kusindika maziwa(Meatu).
“Maafisa
Maendeleo ya Jamii wangu walishirikiana na Wakurugenzi wakabaini fursa
mbalimbali kwenye maeneo yao na vikundi
vya vijana ambavyo kwa sasa vinaendesha miradi ya viwanda kwa kushirikiana na
Halmashauri, kiwanda cha kutengeneza chaki kilichopo Maswa na kingine cha
kusindika maziwa kipo Wilaya ya Meatu” alisema.
“Nawashauri na
ninyi mfanye vitu vitakavyofanya mtambuliwe, fanyeni yale yanayogusa shida za
wananchi, mkifanya hivyo wananchi watawatambua, viongozi watawatambua na Mungu
pia atawatambua” alisema.
Mwenyekiti
aliyeongoza kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii Kanda ya Ziwa ambaye ni Afisa
Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya Serengeti, Ndg.Wambura Sunday
amesema maafisa hao wanafanya jitihada mbalimbali katika maeneo yao na wanaiomba
Serikali iwasaidie kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji
wao.
Aidha, Wambura
amesema kikao chao kimependekeza uanzishwaji wa Chama cha wana taaluma ya
Maendeleo ya Jamii Tanzania ili kudhibiti ubora na viwango vya utoaji huduma
katika Taaluma ya Maendeleo ya Jamii.
Imeharirirwa na Mathias Canal, www.wazo-huru.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment