Na Mathias Canal
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule amewasihi wanaume kote nchini kushikamana katika ujenzi wa Taifa kupitia vikundi kwani kufanya hivyo ni njia imara ya mafanikio katika umoja.
Mhe Senyamule ameyasema hayo wakati akizungumza na wanaume walioanzisha kikundi chao kwa ajili ya ahughuli za kujipatia maendeleo.
Dc Staki amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakijishughulisha peke yao huku wakiamini kuwa vikundi huanzishwa maalumu kwa ajili ya wanawake pakee jambo ambalo sio kweli.
Dc Staki ameeleza hayo wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kikundi cha wanaume cha Wilayani Same (KIWAMA) Kikundi Cha Wanaume Majevu.
Shughuli hiyo iliambatana na upandaji wa miti kama ilivyoamuriwa na Mkuu huyo wa Wilaya Juu ya wajibu wa kila mwananchi katika Wilaya ya Same kupanda miti.
"Kikundi cha KIWAMA ni kikundi cha wanaume majevu, Lakini kwa mazoea hata nilipoalikwa nilifikiri ni kikundi cha wanawake Maana ndiyo tunaowaona kwenye vikundi mara nyingi" Alisema Dc Staki
KIWAMA ni kikundi cha wanaume walioamua kuungana ili kusaidiana katika shida na raha Na kujihusisha zaidi na shughuli za ujasiliamali.
Kikundi hicho kimepania kufanya vizuri katika shughuli za maendeleo bapo wameiomba serikali kuwasaidia kupata mikopo kwa kuwa Halmashauri kwa sasa zina mikopo ya vikundi vya vijana na wanawake tu kwani jambo hilo ni changamoto kwa vikundi vya wanaume ambavyo havitambuliki na serikali.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo amewaahidi kuwaunganisha na idara ya ardhi/na mamlaka ya mji ili wapate eneo la kufanyia shughuli zao za ujasiliamali ambapo wameomba eneo la heka moja.
0 comments:
Post a Comment