Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi wa Maswa
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifuatilia hotuba ya Katibu wa CCM wa Wilaya ya Maswa alipokuwa katika mkutano wa hadhara ili kusikilia na kutatua changamoto ya wananchi wa wilaya hiyo
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo ambako ujenzi wa barabara unaendeshwa ili kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Tawala cha CCM
Licha ya kwamba Wizara ya Madini
kuwa miongoni mwa wizara nyeti katika kufikia uchumi wa viwanda, inakutana na
changamoto nyingi.
Hayo yamebainishwa na Naibu
Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki katika mkutano wa
hadhara na wananchi wa jimbo hilo Tarehe 9 Machi, 2019.
Naibu Waziri Nyongo alizitaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na utoroshwaji wa Madini unaosababisha
Taifa kutokupata kodi stahiki, uwepo wa mikataba isiyolinufaisha Taifa, hali
mbaya ya wachimbaji wadogo na hali ya wachimbaji kufanya shughuli zao bila
kuzingatia suala zima la usalama.
Pamoja na changamoto hizo, Naibu
Waziri Nyongo alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilifanyia marekebisho
ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 mnamo mwaka 2017.
"Mimi pamoja na uongozi
wote wa wizara ya Madini tumepewa dhamana kusimamia sheria hiyo ili Madini
yaliyopo nchini yanufaishe Taifa na watu wake", alisema Nyongo.
Awali kabla ya mkutano huo,
Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo
hilo.
0 comments:
Post a Comment