Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kulia) akiambatana na wajumbe wa Chama na mhandisi wa barabara akikagua ujenzi wa Barabara ya km 1.5 ikiwa ni moja ya ahadi za chama
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Maswa Mwl. Mathius Filagisa akizungumza jambo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofanywa na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo (kushoto).
Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki akiongea na wananchi wa jimbo hilo mara baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo ili kusikiliza kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi
Katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi
na utekelezaji wa ahadi za chama kwa wananchi, Naibu Waziri wa Madini ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo leo amekagua utekelezaji
wa miradi ya maendeleo katika jimbo lake.
Nyongo alitembelea mradi wa ujenzi wa shule
unaoendelea katika kata ya Nyalikungu na kuagiza shule hiyo ya msingi ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwezi
huu ili kuwapa nafuu wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kutafuta elimu.
Aidha, Nyongo ameelekeza mwenge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania utakapopita katika wilaya ya Maswa, ndipo shule hiyo
ifunguliwe rasmi ili kuruhusu masuala mengine ya kimaendeleo kutekelezwa.
Mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika eneo
hilo, Nyongo alielekea katika kijiji cha
ambako alikagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ambao haukuwa
wakuridhisha aidha, alitembelea hospitali ya Wilaya ya Maswa kujionea eneo
lililopendekezwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ambalo mchakato
wa ujenzi na upatikanaji wa pesa umekamilika.
Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo
katika eneo hilo la shule, Diwani wa Kata ya Nyalikungu, Joseph Bundara,
alisema ni kutokuwa na barabara, huduma ya maji, umeme pamoja na ombi
lakujengewa nyumba ya mwalimu ili kuishi karibu na mazingira ya shule.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa
shule iliyopo katika kata hiyo ya Nyalikungu Katibu wa CCM wilaya ya Maswa Mwl.
Mathius Filagisa alimtaka Diwani wa kata hiyo kuhakikisha wakati wa ziara za viongozi
wa juu wa Chama na CCM viongozi wote na watendaji wote wa Serikali wawepo
katika ziara na mikutano ili kujibu
hoja zitakazoibuka wakati wa mikutano hiyo.
Tunatekeleza Ilani ya CCM kuleta makaimu
kwenye ziara za waheshimiwa haifai mjitahidi mwaunge mkono viongozi wenu wakati
wa utekelezaji wa majukumu yao wawapo majimboni” alikazia.
0 comments:
Post a Comment