Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa
kampuni ya NINAYO Jack Langworthy akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo
na shirika lisilo na kiserikali la Heifer utakaowawezesha wakulima
kufikia masoko kupitia njia ya mtandao wa www.NINAYO.com .Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya.
Meneja uendeshaji wa kampuni ya NINAYO
Bovan Mwakyambiki akiungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu
ya kuanzisha ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisolo na
kiserikali la Heifer International Tanzania utakaowawezesha wakulima
kufikia masoko kupitia njia ya mtandaowww.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.
Mkurugenzi mkazi wa Heifer nchini Bi.
Leticia Mpuya akiungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya
kuanzisha ushirikiano baina ya shirika hilo na kampuni ya NINAYO
utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao wa www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.
Tarehe 22 Machi 2017, Dar es salaam.
Kampuni ya Ninayo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la
Heifer International Tanzania ambalo limejikita katika kuondoa umasikini
na matatizo ya njaa leo wameshirikiana katika kuwasaidia wakulima wa
Tanzania kupata taarifa zote zinazohusu mauzo au manunuzi ya mazao
mbalimbali kupitia mtandao wa Ninayo.com.
Ninayo ni jukwaa la mtandao wa
kibiashara unaowawezesha wakulima kuuza, kununua au kuangalia bei
elekezi za mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo pia kuwapa uwanja mpana
wa kulifikia soko la bidhaa hizo kwa urahisi.
Njia hii ya mtandao imejikita katika
kutatua mambo makubwa matatu ikiwemo tatizo la kushindwa kwa mkulima
katika usambazaji ambapo wanunuaji/wateja hawafahamu ni mazao ya aina
gani wakulima wanauza, Mahitaji yasiyofahamika ambapo wakulima
hawafahamu ni kiasi gani wanunuaji wapo tayari kununua mazao yao na
kukosekana kwa utaratibu wa kuwaunganisha wanapohitaji kufanya biashara
za mazao yao.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa habari jana jijini Dar es salaam, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Ninayo Jack Langworthy alisema matumizi ya intaneti
yanazidi kukua kwa kasi sana nchini Tananzia, na hivi sasa intaneti
imesambaa hadi vijiji maskini.
“Tunashukuru kwa kukua kwa kasi ya
mitandao hasa kupitia simu za mkononi, ni uvumbuzi ambao umeleta
mapinduzi katika kila sekta duniani, kuanzia kwenye bishara ya teksi,
hoteli na zaidi sasa inaweza kupatikana kwa wakulima katika masoko ya
Tanzania kukabiliana na mahitaji mahitaji mbalimbali ya chakula kwa bei
elekezi kwa watu wote na hivyo kupunguza upotevu wa mazao mbalimbali”.
Ninayo itasaidia kuwaunganisha wakulima
kwa pamoja katika soko rasmi, na itaweka bei elekezi kwenye biashara ya
mahindi, maharage, ndizi, maembe, matikiti maji pamoja na bidhaa
nyingine nyingi za kilimo katika kuleta uwazi na ukweli wa bei ya soko
na hivyo kuwawezesha wakulima kujivunia mazao yao.
Aliongeza kuwa Ninayo mpaka sasa
imefanikiwa kuwaunganisha wakulima wa mikoa kama Iringa, Mbeya, Morogoro
na Njombe pamoja na wanunuaji wa bidhaa zao, jambo lilisaidia kuongeza
kipato chao.
Aliendelea kusema kuwa Ninayo
inaunganisha hadi wakulima wasio na uwezo wa kupata intaneti kwa kupitia
njia ya ujumbe mfupi wa maneno.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Heifer
International Tanzania Bi. Leticia Mpuya alipongeza juhudi zinazofanywa
kupitia mtandao huo akisema itasaidia kuwaunganisha wakulima na wateja
wao nchini na Afrika mashariki yote.
Ushirikiano kati ya Ninayo na Heifer
International ni katika kuelimisha wakulima jinsi ambavyo wanaweza
kunufaika kwa kuuza mazao yao kwa kupitia mtandao huo. Heifer ambao
wanafanya kazi na mamia ya wakulima nchini itawasaidia wakulima wake
kutumia mtandao wa Ninayo ili waweze kujipatia faida kwa kuhakikisha
wanauza bidhaa zao kwa bei za kujiridhisha.
“Kama shirika linalohusika na kutokomeza
njaa na umaskini, huwa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali katika
kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kulingana na bei zilizo za
kibiashara na kwa manufaa kwao pia kupata wanunuzi sahihi na hivyo
kupitia mtandao huu utasaidia kusulisha changamoto hiii” alisema.
0 comments:
Post a Comment