Idara mbalimbali za dharura wako kwenye daraja la Westminster mjini London, baada ya shambulizi la tarehe 22 Machi, 2017.
Watu wnne ikiwa ni pamoja na mshambuliaji na polisi, wamepoteza
maisha kwenye daraja la Westminster katikati mwa mji wa London kufuatia
milio ya risasi iliyosikia mapema siku ya Jumatano mchana karibu na
jengo la Bunge la Westminster. Polisi inachukulia tukio hilo kama
shambulizi la kigaidi.

Kwa mujibu wa mashahidi, kulisikika
angalau risasi nne. Polisi waliotumwa katika eneo la tukio wamesema kuwa
kuna mtu mmoja ambaye alipigwa risasi.
Kwa mujibu wa chanzo cha usalama watu
wengi wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanafunzi watatu, raia wa
Ufaransa. Tukio hilo lilitokea nje ya jengo la Bunge, karibu na daraja
katika ya eneo hilo ambapo basi pia iliwajeruhi wapita njia.
Polisi akitoa ulinzi nje ya nje ya jengo
la Bunge wakati wa milio ya risasi kwenye daraja la Westminstermjini
London, nchini Uingereza Machi 22, 2017.
Kwa mujibu wa msemaji, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May "anaendelea vizuri".
Bi May alizungumza mbele ya wabunge
mapema mchana lakini msemaji wake amekataa kuthibitisha kama alikua
katika jengo la Bunge la Westminster au karibu na jengo hilo wakati wa
shambulio.
Idadi ya hatua za usalama zimechukuliwa na mamlaka ambayo imesitisha matembezi na utalii.BBC
0 comments:
Post a Comment