Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin
Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi kwa
kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya
Ukimwi.
Amesema Utafiti huo utaangazia pia
kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya
Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.
Amesema Tafiti tatu zilizotangulia
zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti na
utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa kipekee ambapo kwa mara ya
kwanza wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa watahusihwa.
Kwa upande wake, Meneja Takwimu Mkoa wa
Tanga, Tonny Mwanjoto, aliwataka Makatibu Tawala kuhakikisha wanatoa
elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi shuleni kutokomeza maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi.
Alisema kufanya hivyo itasaidia juhudi
za Serikali kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ikiwa na pamoja na
kuyatokomeza moja kwa moja.
Wajumbe wa mkutano wa Wadau wa Utafiti
wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi 2016 /2017 wakifuatilia mada
zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Makatibu Tawala kutoka Wilaya za Tanga na
Wawakilishi wa TACAIDS pamoja na Wadau wa Maendeleo uliofanyika leo
ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.
Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga, Tonny
Mwanjoto akizungumza na waandishi wa habari wa Tanga mara baada ya
kuisha kwa mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashria na Matokeo ya Ukimwi
2016/ 2017.
blog ya kijamii ya tangakumekuchablog, 0655 902929
0 comments:
Post a Comment