METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, January 31, 2023

SERIKALI YATAKIWA KUWAPATIA WAKULIMA TEKNOLOJIA ZA KISASA ILI KUPUNGUZA ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA

Na Doreen Aloyce

Serikali imetakiwa kuwawezesha wanawake hususani kwenye kilimo kwa kuwapatia teknolojia za kisasa za kilimo  mbalimbali zinazoweza kupunguza athari ya mabadiliko ya Hali ya hewa ambazo zitasaidia  kuinua kipato chao na Taifa kwa ujumla. 

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Dr. Mkupete Jaah ambaye ni Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampus ya Mkwawa Idara ya uchumi wakati alipokuwa Kwenye  mkutano na wadau wa kilimo  kuwasilisha tafiti zilizofanywa juu ya  Athari za hali ya hewa kwenye kilimo na jinsi gani ya kukabiliana nazo.

Pia tafiti hiyo imeonesha kwamba upatikanaji na utumiaji wa techologia za kilimo zina uwezo mkubwa wa kupunguza tofauti ya kipato kati ya wanawake na wanaume wanaojihusisha na kilimo.

Daktari Jaah amesema hatua hiyo ni baada ya kufanya utafiti uliofanyika kuanzia mwaka jana januari  2022 mpaka Disemba ambao ulibaini wanawake wengi wanaojihusisha na kilimo wana changamoto ya vitendea kazi kutokana na vipato  tofauti na wanaume.

Amesema kuwa Utafiti umeonesha kwamba wanawake wakitumia teknolojia hizo ikiwemo mbolea na vifaa ,wanafanikiwa zaidi kuliko mashamba ya wanaume lakini wasipotumia hizo teknolojia wanaume uwa na kipato kikubwa asilimia 24.

Serikali ikiwekeza kwa wanawake watanufaika kuwasomesha watoto wao na kuwapa lishe bora ambayo itasaidia kuondoa udumavu kwa watoto ,kuondoa umasikini , kutunza familia na  kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii inayowazunguka.

"Ni vyema serikali iangalie namna ya kuwasaidia wanawake kuwapatia Ruzuku kununua mbolea ambayo itawasaidia kulima na kupata mazao bora hii itawasaidia kujikomboa kiuchumi."

"Lakini pia utafiti wetu umebaini wanawake wengi hawapati mikopo ya kujiendesha kilimo tofauti na wanaume jambo ambalo wengi wamekuwa hawavuni mazao ya kutosha.

Kuwa maafsa ugani wanapaswa kuwatembelea vijijini kuwafundisha namna ya kutumia Kilimo cha Teknolojia kwani imebainika wengi wanalima bila kuwa na utaalamu wa kutosha na kupelekea mazao yao kuharibika.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya kisera kutoka Wizara ya Kilimo , Monica Kanawala amesema kuwa utafiti uliowasilishwa utaleta tija kwa serikali kwani umebainisha changamoto ambazo zinamuumiza mwanamke tofauti na mwanaume. 

Amesema kuwa Serikali kupitia sera zake ikiwa ni sera ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 pamoja na mikakati iliyopo inaendelea kutoa jitihada za kuwezesha upatikanaji wa pembejeo, zana za kilimo na teknolojia za kisasa ambazo zinamuwezesha mwanamke kuweza kishiriki kwenye kilimo pasipo kuumizwa.

"Lakini pia serikali yetu inaendelea kutoa mbolea kwa Ruzuku kwa ajili ya kumsaidia mkulina na upatikanaji wa mbegu bora ambazo zitamsaidia mkulima anufaike na kilimo, "

Kwa upande wake mdau wa  sekta binafsi na mkulima  Idd Senge  amesema utafiti huo utasaidia kuwainua wakulima na kuongeza uelewa wa matumizi ya teknlojia hasa kilimo biashara ambao  bado ni mdogo sana kwa jamii nzima wakiwemo wanawake. 


Kuwa licha ya serikali kuweka mikakati ya kuwasaidia wanawake inapaswa itafute mbolea ambayo haitaleta madhara kwenye ardhi kwani wakulima wengi wanaogopa kutumia mbolea za viwandani kwa madai yanaharibu ardhi na inawalazimu kuitumia kila mwaka ambayo upelekea wenye vipato duni kushindwa. 

"Ni kweli tunashauri Kuwa serikali iwekeze kwa wanawake kuwapatia teknojia za kisasa lakini kuna haja ya kutoa elimu kwa  jamii nzima ili kuondoa wimbi la umasikini  kutokana na uwezo wa kupata mahitaji hasa kununua vifaa."amesema Senge

Kuwa Wananchi wana uelewa mkubwa juu ya mbolea ya viwandani na wanaogopa kuzitumia kwa madai zinaharibu ardhi na wengi utumia ile ya kunyunyizia na sio ya ardhini wakiogopa gharama za  kila mwaka ambayo uwalazimi waweke mbolea kutokana na kipato chao kuwa Duni.

"Lakini pia niiombe serikali isipuuzie huu utafiti kutoka kwa wataalamu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, serikali iwasaidie wakulima kiujumla kuwapatia mbolea ambayo haina madhara ambayo  itasaidia kutunza mashamba kwa kipindi kirefu itasaidia hata wanawake kuitumia vyema.

Mwisho.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com