Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kabla ya kuzindua Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai tarehe 31 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuzindua Tume hiyo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika Mhe. Mussa Azan Zungu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Mhe. Eng. Hamadi Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Zena Said pamoja na Wajumbe wa Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Katibu wa Sekretarieti ya Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za Haki Jinai kuendesha na kusimamia haki jinai kwa kuzingatia misingi ya sheria, weledi, usawa, uadilifu pamoja na mila na desturi zetu.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akizundua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Chamwino.
Aidha, Rais Samia amesema Tume hiyo imeundwa kutokana na kuvurugika kwa mifumo ya haki jinai ambayo inachangiwa na kupuuzwa kwa mifumo ya maadili na hivyo kusababisha baadhi ya wananchi wasio na uwezo kupoteza haki zao.
Taasisi zitakazofanyiwa tathmini na Tume hiyo ni Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Magereza pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Rais Samia pia ameiagiza Tume hiyo kupitia na kuangalia mifumo ya utendaji ya Taasisi hizo na kufanya mabadiliko ya mafunzo, mifumo ya ajira, matumizi ya TEHAMA pamoja na fikra za kiutendaji na mahusiano kati ya taasisi hizo na raia.
Vile vile, Rais Samia amezitaka taasisi hizo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa.
Tume hiyo yenye Wajumbe 12 itaanza kufanya kazi kuanzia tarehe 01 Februari hadi tarehe 31 Mei, 2023.
0 comments:
Post a Comment