METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 9, 2017

MAAZIMIO YA BARAZA KUU MAALUMU LA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA





Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo Alhamis tarehe 9/03/2017 umefanya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa Maalum chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis (MCC)(MB) katika Hotel ya Royal Village Hotel Mjini Dodoma.

Kikao kwa kauli moja kimepitisha na kuridhia mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi Toleo la 1977 marekebisho ya 2017 na kupeleka katika Vikao vya Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa hatua zinazoendelea.

“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itakuwa na uwezo kwa kushauri, kutoa maagizo ya jumla na maelekezo maalum kwa Jumuiya zinazoongozwa na CCM”.

“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itathibitisha Kanuni/Katiba ya kila Jumuiya inayoongozwa na CCM marekebisho yake kabla ya kutumika”. Katiba ya CCM ya 1997 Toleo la 2012 uk. 191 kifungu (4) na sura ya (5).

Kufuatia kikao Maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM na kuzingatia mambo yafuatayo:-

Mabadiliko ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake yana lengo la kukiimarisha Chama chetu ili kuzidi kuziteka hisia, mioyo na fikra za Watanzania walio wengi kwa nia ya kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika lengo lake la kushika dola na kuleta maendeleo endelevu.

Kupunguza idadiya wajumbe ili kuwa na michango makini kwenye vikao vyetu ili kuweza kuwajengea na kuwatetea Vijana wakulima na wafanyakazi na wale walio katika sekta binafsi ili wanufaike na masuala ya Kiuchumi, kijamaii na Kisiasa kulingana na fursa zilizopo kama zilivyoainishwa na kuelekezwa na sera za CCM katika misingi ya kujitegemea.

Mabadiliko haya yatasaidia sana kupunguza migogoro isiyo na msingi katika Jumuiya inayotokana na Vikao vya Kikanuni.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unaahidi kwa CCM kufanyia kazi maagizo na maelekezo yote yatakayotolewa kwa lengo la kufikia kwa vitendo dhana ya CCM mpya, Tanzania mpya wakati Jumuiya hiyo ikielekea kutimiza miaka 40 toka kuzaliwa na kumepiga hatua kubwa za mafanikio Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Mwisho UVCCM imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa umakini, uhodari, ushupavu na kusimamia vyema Ilani ya Uchaguzi wa CCM sambamba na azma yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com