METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 9, 2017

WAFANYABIASHARA NA WANANCHI WATAKIWA KULIPA USHURU WA HUDUMA "SERVICE LEVY"

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawatangazia wafanyabiashara na wananchi wote kuwa wanapaswa kulipa ushuru wa huduma "Service Levy" ambao ni 0.3% ya mauzo.

Tangazo hili linawahusu wamiliki wote wenye Nyumba za kupangisha na maduka ya biashara yanayotambulika kwa majina binafsi.

Malipo hayo yatatozwa kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa ya mwaka 1982 sura ya 290 na marekebisho ya sheria ya mwaka 2012 na sheria ndogo za Halmashauri ya mwaka 2015 ikiwa biashara haina hesabu rasmi utapaswa kulipia viwango mlingano (Flat Rate) vilivyopangwa.
 
Tafadhali hakikisha unalipia ushuru huu Mara moja.

Hatua Kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakao kaidi agizo hili.

Imetolewa na:

John L. Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com