Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya
Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini
Waziri Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini
Uhai, jijini Dar-es-Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mh Ummy Mwalimu (katikati) na Dr Hussein Kidanto - kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma za kinga Wizara ya Afya (kushoto) wakishauriana na Mkurugenzi mtendaji wa Thamini Uhai, Dr Nguke Mwakatundu (Kulia) wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, jijini Dar-es-Salaam
Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya
Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakishauriana wakati wa
mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, jijini Dar-es-Salaam
Tokea 2008, Thamini Uhai imesaidia vituo
vya huduma za afya 19 na zahanati 18 katika mikoa mitatu, na hivyo
kujenga mfumo utakaokuwa mfano bora na inayoweza kutumika kokote nchini
kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga.
(Februari 15, 2017, Dar es Salaam,
Tanzania) – Leo jijini Dar-es-Salaam, Thamini Uhai imetoa mrejesho wa
shughuli zake tokea kuanzishwa kwake na kuwasilisha mipango yake kwa
mwaka 2017 kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Thamini Uhai (iliyoitwa World Lung
Foundation hapo awali), imefanya kazi kwa karibu na wahisani pamoja na
serikali za mikoa, kujenga mfumo ambao umepelekea ugatuzi wa huduma za
dharura za kuokoa maisha ya mama na watoto wachanga kutoka hospitali
kwenda kwenye vituo vya afya. Mfumo huu wa kipekee wa huduma ya afya
umehusisha pia kuboresha vituo vya huduma za afya ili viweze kutoa
huduma hizi za dharura, kuendeleza mafunzo ya jamii kupitia vyombo vya
habari na waelimishaji jamii ili kuhamasisha jamii itumie vituo vya
huduma za afya, kuboresha mifumo ya rufaa, kuhakikisha upatikanaji wa
ushauri wa afya kila wakati. Pia shirika imetoa mafunzo, usimamizi na
elimu endelevu kwa wahudumu wa afya, waganga wasaidizi (AMO) na manesi
ambapo elimu hiyo inatolewa na madaktari bingwa ili kugatua huduma na
ujuzi na hivyo kuongeza uwezo katika jamii zilizopo pemebezoni.
Akizungumzia mafanikio yao, Dr. Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai, amesema:
“Moja ya mafanikio yetu muhimu ni jinsi
shughuli zetu zimeweza kuleta mabadiliko katika maisha ya wagonjwa
katika nyanja zinayotuhusu. Tumeona vifo vya uzazi na rufaa zikipungua
kwa kiasi kikubwa na kwa njia endelevu katika maeneo haya, pamoja na
kuona ongezeko la maana katika idadi ya wanawake wanaoamua kujifungua
katika vituo vya huduma za afya.”
Akitilia mkazo baadhi ya changamoto, Dr.
Mwakatundu ameeleza kuwa ili mafanikio haya yawe endelevu kuna haja ya
kupanga rasilimali za kutosha kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na
kuboresha mfumo wa usamabazaji wa vifaa na madawa.
Waziri wa Afya, Mh, Ummy Mwalimu akitoa
mchango wake kuhusu kazi za Thamini Uhai, amesema: “Ningependa kutambua
mchango wenu katika kuhakikisha akina mama wanajifungua kwa usalama
katika mikoa husika. Naelewa kuwa mmefanya kazi kubwa kuboresha mifumo
ya huduma za dharura katika vituo vya afya na hospitali, mmeanzisha
kampeni za mawasiliano na kuimarisha mifumo ya rufaa kutoka vituo vya
afya kwenda hospitali.”
Thamini Uhai imekwisha kabidhi
serikalini shughuli zake za mradi wa afya ya uzazi katika mikoa miwili –
Morogoro na Pwani, na imepanga mwaka 2017 kuanza utaratibu wa kukabidhi
shughuli zake katika mkoa wa Kigoma.
Kuhusu Thamini Uhai
Tangu mwaka 2008, Thamini Uhai (zamani
iliyojulikana kama World Lung Foundation Tanzania) imefanya kazi ili
kusaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga na kuboresha
upatikanaji wa huduma bora za uzazi wa dharura (CEmONC) katika jamii,
hasa katika maeneo ya vijijini na sehemu zilizo pembezoni ambapo
wagonjwa awali walikuwa wanasafiri masaa tatu au nne kwenda hospitali ya
karibu.
Mpango mkakati wetu ni kusaidia mawasiliano bunifu na kampeni
za jamii ili kuongeza matumizi ya vituo vya afya na uzazi wa mpango;
kuboresha miundombinu; na kutoa mafunzo na kusaidia kliniki zisizo na
daktari kutoa huduma ya uzazi wa dharura. Kwa mikoa Kigoma, Morogoro, na
Pwani:
- Thamini Uhai imeboresha kikamilifu, kukarabati au kujenga upya vituo vya afya 15 vijijini na hospitali za wilaya na inasaidia vituo 5 zaidi. Pia inasaidia zahanati 18 katika maeneo ya vyanzo vya maji, kuboresha upatikanaji wa mahudhurio ya uzalishaji wenye ujuzi kwa ubora wa juu na huduma za uzazi wa dharura na watoto wachanga.
- Zaidi ya wasaidizi 100, waganga wasaidizi, nesi-wakunga, na maafisa wa kliniki wamepata mafunzo ya kina kuhusu huduma ya uzazi wa dharura au nusu kaputi.
- Matumizi ya kituo cha afya kwa ajili ya uzalishaji yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka wanawake 21,661 waliojifungua katika vituo vinavyoungwa mkono mwaka 2011, hadi wanawake 26,189 waliojifungua mwaka 2015.
Mpango huu umepokea msaada wa kifedha
kutoka Bloomberg Philanthropies, Blue Lantern, Fondation H & B
Agerup, na Svenska Postkod Stiftelsen na Thamini Uhai ni mshirika wa
Vital Strategies.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti: www.thaminiuhai.or.tz or Twitter @ThaminiUhai, or Facebookhttps://www.facebook.com/ThaminiUhai/
Maria Sarungi-Tsehai, msarungi-tsehai@vitalstrategies.org, +255 784235215
Kuhusu Vital Strategies
Vital Strategies ni shirika la kimataifa
linalojishughulisha na masuala ya afya na linalenga kusaidia kuongeza
kasi ya maendeleo katika kupambana na magonjwa yenye athari kubwa
duniani.
Timu yetu inatumia mikakati iliyojikita
katika ushahidi na uvumbuzi ili kubuni na kutekeleza sera nzuri za afya
ya umma, kusimamia mipango kwa ufanisi, kuimarisha mifumo ya data,
kufanya utafiti, na kubuni kampeni ya kimkakati ya mawasiliano kwa ajili
ya sera na mabadiliko ya tabia.
Kwa taarifa zaidi au kupanga mahojiano
na mtaalam wa afya ya jamii au afya ya uzazi kutoka Vital Strategies,
tafadhali wasiliana na Tracey Johnston, Vital Strategies, at +44.7889.081.170 autjohnston@vitalstrategies.org
0 comments:
Post a Comment