Baadhi ya washiriki katika mkutano wa maendeleo ya mkoa (RCC)wa Arusha kama wanavyonekana pichani.
Aliyeshika kipaza sauti ni mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli akiwa anachangia mada katika mkutano huo wa( RCC)mkoani Arusha.
Na.Vero Ignatus Arusha.
Jamii za wafugaji katika mkoa wa Arusha
wameshauriwa kubadili mfumo wao wa maisha ili kutojikaribishia baa la
njaa litakaloathiri ustawi wa jamii zao.
Hayo yameelezwa na washiriki mbalimbali
ambao wamehudhuria kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) ambacho
kimewashirikisha wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha pamoja na
wakurugenzi.
Akichangia mada mkuu wa wilaya ya
Longido bwana Daniel Chongolo amesema jamii ya wafugaji wamekariri
katika wilaya wilaya hiyo,chakulakilichopo nimahindi ambapo
wangeliweza kutojishughulisha kutafuta vyakula vingine kama viazi, mtama
na ndizi ambazo vinapatikana kwa wingi kwenye minada hasa ile ya Nanja
na Selela.
Pia ameshauri jamii za wafugaji kua na
utaratibu wa kujiwekea akiba ya chakula hasa wakati ule bei ya mifugo
iko juu kwani wanaweza kuuza sehemu ya mifugo yao na kununua chakula cha
kutosha na kuhifadhi katika maghala ya umma yaliyopo wilayani humo.
Hoja hiyo imeonekana ikichangiwa na
wakuu wa wilaya zingine ambapo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro amesema
katika utafiti aliofanya katika wilaya yake kwenye minada mbalimbali bei
ya mahindi imepanda kutofautisha na vyakula kama ndizi na viazi, kwakua
jamii hizi hazina mazoea ya kula vyakula basi hulalamika ya kwamba kuna
baa la njaa.
Akichangia mjadala huo mkuu wa mkoa wa
Arusha amewataka wadau hao wa mkoa kuwa huru kuchangia, kushauri na
kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa wao.
Kikao hicho kitaendelea tena kesho katika ukumbi wa mikutano wa mkoa.
0 comments:
Post a Comment