Meneja
anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti jeupe)
akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango hatua za
mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji
kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda hicho.
Wataalam
kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa
Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika
kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani
Pwani.
Meneja
anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi pamoja na wataalamu
kutoka Tume ya Mipango wakiwa wameshika vichupa vidogo vinavyotanuliwa
kwenye mitambo na kuwa chupa kubwa za kufungashia kunywaji aina ya
Energy.
Bidhaa ya vinywaji aina ya Energy katika hatua za mwishoni za uzalishaji.
Bidhaa
zikiwa zinapangwa baada ya kupitia hatua mbalimbalikatika katika kiwanda
cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
Baadhi ya
mitambo ya kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la
Mwandege Mkoani Pwani. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO
Na Adili Mhina, Pwani
Tume ya
Mipango imetembelea kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la
Mwandege Mkoani Pwani na kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji
za kiwanda hicho ikiwa ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya
Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Timu ya
wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango
ilifanya mazungumzo na Meneja anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani
hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika
hali nzuri na kinaendelea na shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora
unaotakiwa katika kukidhi mahitaji ya soko.
Bibi
Mwashigadi alieleza kuwa kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi
800 ambapo kati hao 500 ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300
ni ajira zisizo za moja kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya
kuendelea kupanua soko la bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza
bidhaa katika nchi za Kenya na Rwanda.
Kuhusu
upatikanaji wa matunda ya kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo
alieleza kuwa hakuna changamoto kwani hapa nchini kuna matunda yenye
ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda na kiwanda chake kinategemea
malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kutoka maeneo
mbalimbali nchini.
Pamoja na
hayo, Bibi Mwashigadi aliongeza kuwa kiwanda chake kimeendelea kununua
matunda kwa bei nzuri ambayo inaendana na bei ya kawaida ya soko lengo
likiwa ni kuhakikisha mkulima anaona faida ya kujishughulisha na kilimo
cha matunda.
Hata
hivyo alitoa wito kwa Tume ya Mipango kuangalia namna ya kutengeneza
sera itakayosaida kumnufaisha zaidi mkulima mdogo kwani kwa sasa
madalali ndio wanaochukua matunda toka kwa wakulima na kupeleka
kiwandani na mkulima anaishia kupata faida kidogo huku madalali
wakiendelea kunufaika.
0 comments:
Post a Comment