Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya
Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF) Hoteli ya Hyatt Regency Dar
es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akihutubia kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Meza kuu.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Salum Mussa (kulia), akishiriki uzinduzi wa mfuko huo na wadau wengine.
Uzinduzi ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati), akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye kwa ushiriki wake katika kuchangia mfuko huo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko.
Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kampuni hiyo ilichangia sh.milioni 100.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga kwa ajili ya kuchangia mfuko wa ukimwi Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko.
Makamu wa Rais akipeana mkono na mdau aliyeshiriki uzinduzi huo.
Meneja Mawasiliano Msaidizi wa Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza baada ya kutoa mchango wa sh. milioni tano.
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU
wa Rais Samia Suluhu Hassan ameendesha harambee ya sh. bilioni 1,036,
050,000 ahadi ikiwa ni sh. bilioni 5, 913,650,000 pamoja na ahadi ya
serikali kwa ajili ya Mfuko wa Ukimwi Tanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Ukimwi (ATF) ulioenda
sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani jijini Dar es Salaam
juzi, aliwaomba wadau mbalimbali kuchangia mfuko huo ili kukabiliana
na changamoto ya ukimwi nchini.
"Tunaomba
wadau mbalimbali kusaidia mfuko huo kwani bado tunachangamoto kubwa ya
ugonjwa wa ukimwi" alisema Makamu wa Rais mama Samia.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama Sera ya ukimwi ya mwaka 2001 imeelekeza
kuanzishwa kwa mfuko wa ukimwi ambapo serikali ilianza mchakato wa
kuanzisha mfuko huo mwaka 2008.
Alisema mfuko huo umeanzishwa kwa kupitia marekebisho ya Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi namba 6 ya mwaka 2015.
"Madhumuni
makubwa ya mfuko wa Ukimwi ni kuhakikisha uwepo wa rasilimali za
kutosha na za uhakika katika kupambana na ukimwi zilizotokana na mapato
ya ndani" alisema Mhagama.
Alisema
kulingana na Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi
uliothaminishwa, mahitaji ya Taifa kugharamia Ukimwi katika kutekeleza
makakati huo kwa kipindi cha miaka mitano 2013/14 na 2017/18
yanakadiriwa kufika 6 Trilioni (USD 2.975 bilioni).
Alisema
asilimia 93 ya fedha hizo zinatarajiwa kutoka kwa wafadhili na asilimia
7 kutoka vipato vyandani na kuwa sehemu kubwa ya asilimia 56 ya fedha
zote katika miaka hiyo mitano ni kwa ajili ya manunuzi ya dawa za
kufubaza VVU (ARV drugs)
Alisema
mahitaji ya fedha katika kipindi cha mwaka 2016/17 ni Trilioni 1.258,
fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 833 na hivyo kuwa
na upungufu wa Bilioni 425.
Alisema
katika kipindi cha mwaka 2017/18 mahitaji ya fedha ni Tsh. Trilioni
1.260, fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 740 na
hivyo kuwa na upungufu wa Bilioni 520.
Mhagama
alisema licha ya kupungua kwa ahadi ya wafadhili bado hakuna uhakika
kama fedha zilizoahidiwa zitapatikana zote kwa mantiki hiyo hivyo
kuongeza fedha zinazotoka ndani ya nchi ni suala la muhimu sana.
0 comments:
Post a Comment