Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiongea na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
cha Mbeya (MUST) alipowatembelea akiwa mmoja wa wanachuo wa mwanzao
waliohitimu katika chuo hicho ambapo awali kilijulikana na kama Taasisi
ya Sayansi na Teknolojia (MIST). Prof. Ole Gabriel amewahimiza viongozi
hao wawe msatari wa mbele katika kusimamia taaluma na kuwajengea uwezo
wanafunzi wao wajitambue na wawe na utamaduni bora wa kufikiri kimkakati
na usimamizi ili waweze kuendana na ulimwengu wa sasa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akitembelea moja ya karakana wakati wa ziara yake hivi karibuni
katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST).
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia cha Mbeya (MUST) Prof. Joseph Msambichaka mara baada ya kikao
na Menejiment ya chuo hicho wakati wa ziara yake hivi karibuni Mkoani
Mbeya.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) Prof.
Joseph Msambichaka (katikati) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) moja ya
madaftari yake aliyotumia wakati akisoma chuni hapo kikijulikana kama
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (MIST).
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akifurahia zawadi ya moja ya madaftari aliyotumia akiwa
mwanafunzi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (MIST) ambapo kwa
sasa ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST).
Moja
ya vyombo vya usafiri alivyotumia Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa mwanafunzi
katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (MIST) ambapo kwa sasa ni Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST).
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (aliyevaa tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya mkutano wake na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
cha Mbeya (MUST) hivi karibuni mkoani Mbeya.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbeya)
Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
Viongzi
wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) wametakiwa
kuwa imara katika kusimamia taaluma chuoni hapo na kuwajengea uwezo
wanafunzi wa kujitambua na kuwa utamaduni bora wa kufikiri kimkakati na
usimamizi ili waweze kuendana na kasi ya ulimwengu wa sasa wa sayansi na
teknolojia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel amsema hayo alipokuwa akiongea na wajumbe wa Menejimenti ya Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) hivi karibuni
alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya.
Prof.
Ole Gabriel amewaambia wajumbe hao kuwa siri kubwa ya mafanikio ni
pamoja na kutimiza amri ya sita za kufikiri kimkakati na usimamizi
ikiwemo kujenga utendaji bora, kudumisha utendaji bora, kuelewa kazi za
msingi wako, kujua mshindani wako katika kazi unayofanya, kukabiliana na
kasi ya Teknolojia pamoja na kuwa wazi juu ya malengo uliyojiwekea
wakati wote.
Ili
chuo hicho kifikie malengo yake, Prof. Ole Gabriel amewaambia wajumbe
wa Menejimenti ya Chuo hicho kuwa ni vema wawe na utamaduni wa kufanya
tafiti mbalimbali na usimamizi hatua ambayo itakifanya chuo hicho kuwa
bora miongoni mwa vyuo vikuu nchini kwa kutoa wananfunzi wenye ubora
unaohitajika kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Zaidi
ya hayo, viongozi hao wameshauriwa pia kujenga utamaduni wa kuwa
miongoni mwa watu wenye fikra kubwa ambao wanania ya kutengeneza mambo
yatokeee na wasiwe watu wa wastani wenye nia lakini wanaangalia mambo
yatokee wala wasiwe watu wenye akili za kawaida wenye nia lakini
wanashangaa kwanini mambo yanatokea.
Aidha,
Prof. Ole Gabriel amezitaja sifa za mtu anayefikiri kimkakati na
usimamizi kuwa ni pamoja na daima kuona fursa nje ya matatizo, kuwa na
mkakati wa majadiliano, kuripoti matatizo na ufumbuzi mbadala, pamoja na
kufanya maamuzi kwa haraka na kwa usahihi.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha
Mbeya (MUST) Prof. Joseph Msambichaka kwa niaba ya Menejimenti
amemshukuru Katibu Mkuu Prof. Ole Gabriel kuwajali na kuwathamini
ikizingatiwa ni miongoni mwa wanachuo wa mwanzao waliohitimu katika chuo
hicho ambapo awali kilijulikana na kama Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia (MIST).
Akitoa
taarifa fupi ya chuo, Prof. Msambichaka amesema kuwa chuo kwa sasa kina
jumla ya wanachuo 3,852 ambapo idadi ya wanachuo wa wanaume 3,236 na
idadi ya wanawake ni 616 ambao wanasoma katika sehemu nne za chuo hicho.
Sehemu
hizo ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Taasisi ya Uhandisi na
Teknolojia, Shule ya Mafunzo ya Biashara pamoja na Chuo cha Sayansi na
Ualimu wa Ufundi.
0 comments:
Post a Comment