Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM-Bara Rajab Luhwavi, akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Muasisi
wa TANU, Khadija Kamba, katika makaburi ya Kisutu, wakati wa mazishi
yaliyofanyika Jana, Desemba 01, 2016, katika makaburi hayo mjini Dar es
Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
Na Bashir Nkoromo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza mamia ya wananchi katika
maziko ya muasisi wa chama cha Tanganyika African Union (TANU) na
baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khadija Kamba, aliyefariki jana na
kuzikwa Jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kinana
ambaye alifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi,
akitoa salam za rambirambi za Chama, alisema, CCM itamkumbuka na kuuenzi
daima mchango mkubwa alioutoa hasa wakati wa harakati za ujenzi wa TANU
na harakati za ukombozi wa Tanzania wakati wa uhai wake.
"Binti
Kamba alikuwa ni nguzo na chachu muhimu katika kuasisiwa kwa TANU na
mpambanaji aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutafuta Uhuru
wa nchi hii, hivyo Chama kitambukumbuka na kumuenzi daima Mama huyu",
alisema Kinana, wakati akitoa salam za rambirambi wakati wa maziko.
Kinana
alisema, licha ya kuwa muasisi, lakini Binti Kamba kamtika maisha yake,
aliendelea kuwa nwanachama na kada mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi na
kuendelea kuwa kisima cha kuchota hekima na maarifa hadi anafariki
dunia.
Alisema,
kutokana na kuguswa na msiba huo, kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu wa
Chama, ameandaa hitima itakayosomwa keshokutwa katika Msikiti wa Masjid
Quba, kumuombea maghfira.
Binti
Kamba, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 94, alifariki juzi
asubuhi, nyumbani kwa mwanae wa kulea, Kamba Abdallah, jijini Dar es
Salaam, kutokana na kuugua figo na moyo.
0 comments:
Post a Comment