Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza Jambo wakati wa
Kikao chake na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC).
Sehemu ya
Menejimenti ya TPDC wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa Nishati
na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja
na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke (wa pili kushoto) na ujumbe
uliofuatana na Balozi huo.
Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na
Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooken (wa kwanza kushoto) na ujumbe
wake walipomtembelea ofisini kwake Jijijini Dar es Salaam. Kulia ni
Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent
Luoga.
Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na
Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao wakati Naibu Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo amekutana na Bodi na
Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika
kikao kilichochadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na
shirika hilo ikiwemo Mradi wa Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na Mradi wa
Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Katika
kikao hicho Prof. Muhongo ameitaka Bodi na Menejimenti hiyo kuongeza
kasi katika utekelezaji wa miradi husika kutokana na manufaa ya miradi
hiyo kwa Maendeleo ya Taifa.
Mbali na
Bodi na Menejimenti ya TPDC, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Prof.
James Mdoe na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha,
wakati huo huo, Waziri Muhongo pia amekutana na Balozi wa Uingereza
nchini Sarah Cooke ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu sekta ya
nishati ikiwemo chanzo cha Nishati Jadidifu.
Pia,
Waziri Muhongo amekutana na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia
Blaser ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati.
0 comments:
Post a Comment