METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, November 4, 2016

Mazoezi ni Afya kiakili na kimwili

Kwa mwenyeji wa Mwanza naamini wanautambua umbali wa kutoka Pasiansi hadi Airport kupitia jeshini, Nimefanya mazoezi nikitumia jezi ya zawadi niliyopewa wakati nilipojiandikisha Mbio za Ikungi Half Marathon 2016 zilizofanyika Wilayani Ikungi Mkoani Singida.

Nipo hapa Jijini Mwanza na uongozi wa Mkoa wa Singida kuipa sapoti Timu yetu ya Singida United ili iweze kupanda kutoka Ligi daraja la kwanza na kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara.

Ukipewa jukumu ni lazima kujiimarisha kiafya na kimwili adui hakabiliwi na mtu goigli anakabiliwa na Mtu maridani mwenye nguvu na afya ya mwili na Akili.

Singida United leo anamkaanga Alliance Fc katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuwaachia majonzi wenyeji wa Mwanza.

Salaaaam...!
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Mwanza
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com