Na Daudi Manongi
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa
vyombo vya Habari nchini kuwa mbele katika kusimamia Maadili na
kuutangaza Utamaduni wa Mtanzania.
Rais
Magufuli ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahojiano
ya mwaka na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aingie
madaraka.
“Jukumu
la kulinda Utamaduni na Maadili ya mtanzania ni la kila mzalendo,
mtanzania, mzazi na Wizara husika ipo kwa ajili ya kusimamia jambo hili
na vyombo vya habari mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kulisimamia kwa
kuanzia katika vyombo vyenu vya Habari kutokana na kile
mnachoonyesha”Alisema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli amevitaka vyombo vya Habari kuwa wazalendo katika
kutengeneza vipindi vyenye mahadhi ya kitanzania ili kuisaidia jamii
kukua katika utamaduni wetu na kusaidia kujenga maadili yaliyo bora.
Mbali na
hayo Rais Magufuli amezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana
katika kipindi chake cha mwaka mmoja toka aingie madarakani ikiwemo
kuongezeka kwa mapato kutoka bilioni 800 mpaka makusanyo ya shilingi
trilioni 1.5 kwa mwezi.
Pia
amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2016 ya trilioni 29.5 iliyotenga asilimia
40 kwenye miradi ya maendeleo imekuwa yenye mageuzi makubwa
ukilinganisha na bajeti ya miradi hapo nyuma mabayo ilikuwa asilimia 26
tu.
Pamoja na
hayo Rais magufuli amesema kuwa Serikali imeagiza ndege nyingine mbili
zinategemewa kufika nchini mwanzoni mwa mwaka 2018 ili kuboresha sekta
ya utalii nchini.
Akizungumzia
uundwaji wa serikali amesema mategemeo yake katika serikali aliyoiunda
imefanikiwa kwa kuwa Baraza aliloliunda la watu wachache limekuwa la
mafanikio makubwa na hili limetokana na ushirikiano mkubwa wa mawaziri
wake.
0 comments:
Post a Comment