METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 13, 2016

WAZAZI WANA NAFASI KUBWA KWENYE MALEZI YA WATOTO KITAALUMA


Na Creptone Madunda

Maendeleo ya sekta ya elimu yanahitanyi mipango iliyosheheni weledi wa hali ya juu na nguvu ya pamoja katika utekelezaji kutoka kwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo. Mzazi ni mmoja kati ya wadau wadau wa maendeleo ya sekta ya elimu lakini sichelei kusema " Shikamoo wazazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

Mzazi anaamka asubuhi saa 10 mpaka saa 12 akiwaacha watoto wamelala na kurudi nyumbani saa 1 mpaka saa 3 usiku macho yake na akili yake yote kwenye taarifa ya habari, tamthiliya, chakula au kinywaji.

Mzazi huyu atafanya hivyo kwa mwaka mwaka wa kwanza mpaka wa saba, nne au sita. Kibaya zaidi mzazi huyu hajawahi kwenda shule hata siku moja kuulizia maendelea ya mwanae tangu ampeleke kuanza darasa la kwanza, kidato cha kwanza au tano, si ajabu kumuona siku ya graduation akija na keki, mataji bila kusahau wapambe akiwa amewajaza kwenye yutong.

Kutokana na hali iliyopo kwa wazazi kukaa mbali na walimu, siasa kuingia kwenye elimu, kuporonyoka kwa maadili kutokana na kukua kwa teknolojia, kupondeka kwa walimu kutokana na changamoto na mazingira magumu ya kazi yao tutegemee nini katika mustakhabali wa maendeleo ya taifa letu na kizazi cha baadaye ?

Wengi waweza kubisha na kuibuka na maswali na mabishano yasiyo na mwisho, tunaweza kujiuliza maswali machache katika msingi wa mada iliyopo mezani:

(a) Pindi ulipokuwa shule ni mara ngapi mzazi wako alifika shule kuulizia na kujadiliana na walimu kuhusu maendeleo ya taaluma yako ?

(b) Je unafanya kazi ambayo ilikuwa ni ndoto ya maisha yako ?

Kama jibu NDIO ni jambo la heri na la kumshukuru Mungu, walimu wako pamoja na wazazi wako.
Kama jibu ni HAPANA ni jambo la kuwalaamu:

- WAZAZI wako kwa kushindwa kukusimamia kuhakikisha unafikia lengo.

SERIKALI hasa Wizara ya elimu na tume ya vyuo vikuu kwa kukupangia kusoma kozi au masomo ambayo hayajawahi kuwa ndoto yako.

WEWE MWENYEWE unahitaji kujilaumu kwa kushindwa kusimamia mipango yako ili kutimiza ndoto ya maisha yako.

(c) Kwa mzazi wa aina hii anaweza kusimama nakusema tabia ya mwanangu ni nzuri au mbaya ?
Ndugu zangu shule sio jalala kwani hata jalala kwani hata jalalani huwa tunatembelea na kukusanya taka na kuzichoma moto.

Shule sio jela kwani hata jela huwa tunafika kuwatembelea wapendwa wetu wanaotumikia vifungo mbalimbali.

Kwanini wazazi mnashindwa kufika shule na kuwatembelea watoto wenu na kujua maendeleo yao kitaaluma?

"NA NDIO MAANA WANAFUNZI HUDIRIKI HATA KUWADANGANYA WAZAZI WAO ETI WAMEVUNJA "ASSEMBLY HALL" HIVYO WANATAKIWA KULIPA KILA MMOJA KIASI MTOTO ATAKACHOSEMA NA MZAZI HUTOA FEDHA KWA UJINGA WAKE"
Hamjui kuwa shule ni sawa na uwekezaji mwingine ambao umekuwa ukijiuliza ni kiasi gani umewekeza na kila siku au mwisho wa siku utategemea kupata mavuno kiasi gani na bora kiasi gani?

Ni kiasi gani mnatumia kwa ajili ya sare, chakula, nauli, viandiki, vitabu masomo ya ziada na tripu za mafunzo kwa vitendo au mnatembea na farsafa ya elimu bure mkitegemea miujiza kutokana na farsafa hii ? NO LET US GET UNITED AND WORK TOGETHER.

WALIMU hawawezi kukwepa lawama za kutotoa DIRA na MUONGOZO kwa mwanafunzi mwenye nia na maono ya kufika mbali ili kuweza kutimiza ndoto za maisha yake lakini bila ushirikiano kutoka kwa mzazi, serikali na wadau wengine ndoto hizi za wanafunzi zimekuwa zikiiishia vichwani mwao au usingizini na kutimilika kwa wachache kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com