Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua
Mahakama
moja nchini Uganda imempiga faini ya Shilingi 40,000 za Uganda mbunge
mmoja nchini humo kwa makosa ya kukojoa hadharani.
Kwa mujibu wa
gazeti la Daily Nation nchini Kenya Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa
ya Arua siku ya Jumanne aliwasili mbele ya mahakama ya mji wa Kampala na
kushtakiwa kwa kukojoa katika ukuta wa jumba la wizara ya fedha.
Alikiri kufanya makosa hayo na akaachiliwa baada ya kulipa faini.
Kwa
mujibu wa gazeti hilo Kiongozi wa mashtaka aliiambia mahakama kwamba
mbunge huyo alifanya makosa hayo mwezi Septemba 25 mwaka huu katika
barabara ya Kyaggwe mjini Kampala.
Upande wa mashtaka ulisema kuwa vitendo vya mbunge huyo vilikuwa kinyume na sheria za baraza la manispaa ya Kampala za 2016.
Kukiri kwake kunajiri baada picha kadhaa za yeye akikojoa kando kando ya barabara kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Chanzo-BBC
Wednesday, October 25, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga (Mb) Mwenye Tai, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalish...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Pichani: Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, akizungumza na wakulima na wadau mbalimbali w...
-
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akipita katika moja ya maeneo ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa ...
-
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amefunga mashindano ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment