Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata – (Mwenye
suti ya bluu katikati) pamoja na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw.
Elijah Mwandumbya (Kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na
walipakodi waliofika katika Ofisi Mpya ya TRA Kimara ili kuhakiki Namba
zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN. Ofisi hiyo imezinduliwa leo tarehe
26 Oktoba 2016 na Kamishna Mkuu wa TRA ili kuwafikia wananchi kwa
karibu zaidi na kuboresha huduma mbalimbali za Kodi.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akikata
utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa ofisi mpya ya TRA iliyoko Kimara
Mwisho leo Tarehe 26 Oktoba 2016, Kushoto kwake ni Kamishna wa Kodi za
Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na Wakurugenzi wengine wa TRA
wakishuhudia tukio hilo
Meneja wa
TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande (anayeongea kwa vitendo) akitoa
maelezo ya kituo hicho kipya kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (aliyeketi) wakati wa uzinduzi wa
ofisi hiyo. Wengine kutoka kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw.
Elijah Mwandumbya, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Bw. Abdul Zuberi,
Meneja wa Majengo Gerald Mwikuka, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bw.
Gerald Mwanilwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw.
Richard Kayombo.
:Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata
akisalimiana na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA
iliyoko eneo la Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa
Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akiongea
na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA-Kimara
Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa
uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna
wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya akimweleza jambo Kamishna
Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alipotembelea ofisi mpya za TRA Kimara
Mwisho kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo.
Meneja wa
TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande akimwonesha jambo Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kushoto kwake)
alipotembelea ofisi ya TRA Kimara Mwisho wakati wa uzinduzi huo
uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2016
Katika
jitihada za kuboresha huduma kwa walipakodi na kuzifikisha huduma hizo
kwa karibu zaidi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA)
Bw. Alphayo Kidata amezindua ofisi mpya ya TRA katika eneo la Kimara
Mwisho jijini Dar es Salaam Tarehe 26 Oktoba 2016 itakayotoa huduma zote
za kikodi ikiwemo usajili na uhakiki wa Namba za Utambulisho wa
Mlipakodi –TIN, Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT, Malipo ya
Kodi za Magari, Kodi zote za Mapato zikiwemo Kodi za Makampuni, Watu
Binafsi, Wafanyakazi (PAYE), Kuendeleza Ufundi Stadi – SDL, VAT, Ushuru
wa Stampu na huduma nyingine za kikodi.
Akizungumza
na walipakodi waliofika katika ofisi hiyo kupata huduma wakati wa
uzinduzi, Bw. Kidata aliwashukuru kwa mwitikio wao katika zoezi la
uhakiki wa taarifa za TIN ambao utaisaidia Mamlaka kupata idadi sahihi
ya walipakodi ili kuondoa walipakodi hewa ikiwa ni pamoja na kuboresha
huduma za ulipaji kodi.
“Zoezi hili litaongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi na ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu” Alisema Bw. Kidata
Kamishna
Mkuu wa TRA aliwataka walipakodi hao wanaoishi maeneo ya karibu na ofisi
hiyo mpya ya TRA iliyopo Kimara Mwisho kuendelea kujitokeza kwa wingi
ili kupata huduma mbalimbali za kikodi ikiwemo uhakiki wa taarifa zao
TIN kabla ya tarehe ya mwisho wa zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam
ambayo ni tarehe 30 Novemba 2016.
Aidha
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya alisema TRA
imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma zake na kuwafikia
walipakodi kwa ukaribu zaidi ili kuondoa usumbufu na kuokoa muda wa
upatikanaji wa huduma hizo.
0 comments:
Post a Comment