Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja.
Na.Alex Mathias,Dar es salaam
Baraza la
Michezo la Taifa limeagiza michakato yote inayoendelea kubadilisha
umiliki wa timu kutoka kwa Wanachama kwenda kwenye umiliki wa hisa na
ukodishwaji kwa vilabu vyote vya michezo usitishwe mara moja hadi
marekebisho ya katiba zao kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Michezo la
Taifa na kanuni za Msajili Namba 442 kanuni ya 11 ya kifungo kidogo cha
1-9 yatakapofanyika.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, amesema kuwa
baraza linapenda kuona kwamba wahusika wakuu wa jambo hilo hasa klabu
za Simba na Yanga wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia
malengo yao.
Aidha
amesema kuwa endapo vilabu hivyo kama vitaendelea na mchakato huo kabla
ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki
zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka maelezo hayo.
“Hivi
karibuni imeibuka michakato ya watu wakitaka kubadilisha umiliki wa
vilabu vya wanachama na kuvielekeza kwenye utaratibu wa hisa na
ukodishwaji,vitendo hivi vimesababisha migogoro mikubwa ambayo
inaashiria uvunjifu wa amani ndani ya tasnia ya michezo kwani imefikia
hatua watu wanaenda mahakamani mfano mzuri ndani ya klabu ya
Yanga”alisema Kiganja.
Ameongeza
kuwa makundi ya wapenzi na wanachama wamejikita katika mijadala ambayo
hatma yake ni kuzidi kuibomoa jamii badala ya kuijenga na kuimalisha
michezo nchini.
Aidha
amesema kuwa kuna mipasuko ambao umepelekea baadhi ya wanachama wameona
kuwa hawaridhishwi na mwenendo mzima na pengine hata taratibu za suluhu
zilikiukwa na kuona hazifai na kuamua kukimbilia Mahakamani.
“Kutokana
na hali hiyo BMT kama chombo pekee cha kisheria kilichopewa dhamana ya
kusimamia Michezo nchini,hakiwezi kuvumilia ukiukwaji wa Sheria na
taratibu zinazoendelea na kuashiria kutoweka kwa amani kwenye tasnia ya
Michezo”alisema Kiganja.Hivyo basi,Baraza linasitisha michakato yote
inayoendelea ya kutaka kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwenye mfumo
ulipo sasa na ni vyema vilabu vikaendelea kubaki kuwa mali ya Wanachama.
0 comments:
Post a Comment