watoto wakiendesha baiskeli katika kambi hiyo
Serikali ya ufaransa inasema kuwa wamekamilisha uhamishaji wa maelfu ya wahamiaji katika kambi za Calais, maarufu kama jungle.
Uvunjwaji
wa kambi hizo ulianza siku ya jumatatu huku wahamiaji wakisafirishwa
kwa mabasi katika kambi mbalimbali za wakimbizi nchini humo.
Picha za
televisheni zimeonesha moshi mweusi ukitokea kwenye mahema na duka
ambayo huenda yamechomwa moto na wanaharakati wenye hasira au wahamiaji.
Lakini
mbali na serikali ya nchi hiyo kusema kuwa kambi hiyo sasa haina watu,
Dorothy Sang kutoka shirika la kutetea haki za watoto la save the
children ameiambia BBC kuwa bado kuna wasiwasi juu ya idadi kubwa ya
watoto wasio na wazazi ambao wanadhaniwa kuwepo bado katika kambi hiyo.
BBC
0 comments:
Post a Comment