METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 13, 2016

MSONDO NGOMA FAMILY DAY KUFANYIKA LEKHAM HOTEL BUGURUNI

mson1
Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma Shaban Dede kulia na Hassan Moshi wakiimba jukwaani katika moja ya maonesho ya bendi hiyo jijini Dar es salaam.
mson
Katibu wa kamati ya maandalizi ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed Hussein
Bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini,MSONDO NGOMA MUSIC BAND(BABA YA MUZIKI),inakuletea onyesho lao kubwa la kila mwezi maalum kwa wanafamilia wa Msondo Ngoma na wadau wa muziki wa dansi maarufu kwa jina la MSONDO NGOMA FAMILY DAY,ambalo kwa mwezi huu litafanyika wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Lekham Hotel,Buguruni.

Akiongea na fullshangwe blog,Seneta wa Bendi hiyo ambaye pia ni katibu wa kamati ya maandalizi ya Maonyesho hayo ya kila mwezi Bw.Abdulfareed Hussein,ameeleza kwamba baada ya mafanikio makubwa katika maonyesho yalopita,sasa burudani itaangushwa Lekham Hotel,ikiwa na kauli mbiu ya CHANGIA BENDI YAKO,CHANGIA BIMA YA AFYA KWA WANAMUZIKI WETU.

Katibu huyo pia amefafanua kwamba onyesho la mwezi huu litakuwa maalum la kuchangia upatikanaji wa bima ya afya kwa wanamuziki wa Msondo ngoma.

Bendi hiyo imedhamiria kuja na mipango mbalimbali katika kuendeleza muziki wa dansi na kadri siku zinavyokwenda ndivyo mikakati mbalimbali itakavyotekelezwa.

Katika onesho hilo pia kutakuwa na zawadi kwa mtu atakayecheza vizuri mtindo wa msondo ngoma , atakayeimba vizuri nyimbo ya mashindano ya Msondo Ngoma na atakayependeza zadi katika siku hiyo.
Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni 10,000,japo wadau wanaruhusiwa kuchangia zaidi ya bei hiyo na kwa mawasiliano ya uchangiaji wa awali unaweza kumpata na kukupa maekekezo kupitia namba ya simu 0653909050.

CHANGIA MSONDO NGOMA,CHANGIA BIMA YA AFYA KWA WANAMUZIKI WETU.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com