Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen
Kebwe. Waziri Makamba yuko Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku
mbili.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba, wa tatu kutoka kulia akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa
katika Mto Mambogo
Baadhi ya
wananchi wa Kijiji cha Parakuyo wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kabla ya
kufanya mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Sehemu ya
Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha
Parakuyo Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo
pichani) changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
Sehemu ya
Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha
Parakuyo Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo
pichani) changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
Na Lulu Mussa- Morogoro
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba ameitaka jamii ya watu wa Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa
kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo miongoni mwao kwani ndio misingi
ya watanzania.
Rai hiyo
imetolewa leo katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima
na wafugaji ambazo zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba
alizitaka jamii hizo kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida
ya sasa na vizazi vijavyo.
Miongoni
mwa changamoto zilizobainishwa na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya
mabadiliko ya Tabianchi na athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi
bora ya ardhi.
Waziri
Makamba ameuagiza uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda
kamati ya ‘Amani’ itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za
wakulima na wafugaji na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta
suluhu ya kudumu baina ya pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara
kwa mara. “Undeni Kamati hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo
kwa Kamati husika juu ya namna bora ya kutatua migogoro” alisisitiza
Waziri Makamba.
katika
jitihada za kukuza uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake,
Waziri Makamba ameitaka Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za
Mazingira ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi
kuipati mafunzo Kamati hizo ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo
ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya
maeneo yao.
Aidha,
Waziri Makamba amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu
sana na kuitaka jamii ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu
katika zoezi la kuhakiki na kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi
kiasi gani inahitajika kwa wakulima na kiasi gani kwa wafugaji.
“ndugu
zangu niwasihi, Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na
matumizi bora ya ardhi, hivyo nawashauri mmshiriki kikamilifu katika
zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya mifugo na ardhi iliyopo”
Makamba aliongezea.
0 comments:
Post a Comment