Kaimu
Meneja wa Bandari wa Bandari Tanga, Hendry Arika, (kushoto)
akimtambulisha kiongozi wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wanaowakilisha
nchi zao nchi, Roeland Vande Geer kwa Captain Bandari, Endrew Matiria
wakati ulipofanya ziara yake Tanga kuangalia fursa za uwekezaji baada ya
ujio wa mradi wa Bomba la Mafuta Tanga.
Mabalozi
12 kutoka nchi mbalimbali wamefika Tanga kuangalia furasa za uwekezaji
kwa kutembelea Bandari ya Tanga, Bohari ya mafuta ya GBP na eneo ambalo
litajengwa bombala Mafuta kijiji cha Chongoleani.
Akizungumza
katika mkutano na ujumbe huo, Meneja wa Bandari Tanga, Hendry Arika,
alisema ujumbe huo umejionea kasi kuelekea ujenzi wa bomba la Mafuta na
kuwataka wawekezaji wa ndani kuangalia namna ambavyo nao watawekeza.
Kaimu
Meneja Bandari Tanga, Hendry Arika, akiwafahamisha mabalozi wa nchi za
Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini wakati walipotembelea Bandari ya
Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa mradi wa bomba la
mafuta Tanga.
Mabalozi wakitembelea bohari ya mafuta bohari ya GBP.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji, akiwaonyesha mabalozi wa
nchi 12 za Ulaya wanaoziwakilisha nchini zao nchini ramani ya eneo
litakapojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga ziara
waliyoifanya leo.
Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga, Hendry Arika akizungumza na waandishi wa
habari leo eneo litakalojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani
Tanga wakati wa ziara ya mabalozi 12 kutoka Jumuiya ya Ulaya
wanaowakilisha nchini zai nchini.
Kiongozi wa mabalozi wa nchi 12 Jumuiya ya Ulaya, Roeland Van Geer, akizunguza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mabalozi hao Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa bomba la Mafuta,habari hii kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha.
0 comments:
Post a Comment