Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Serikali ya Gambia imesema kuwa itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na Waafrika pekee.
Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi nchini humo mwaka 1994.
ICC: Kenya ilikataa kushirikiana nasi kikamilifu
Afrika Kusini kujiondoa mahakama ya ICC
Burundi kujiondoa mahakama ya ICC
Uchaguzi
ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka huu viongozi nane
wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa kuhusika
katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limesema kuwa
maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za binadamu
nchini Gambia.
BBC
0 comments:
Post a Comment