METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 4, 2016

DRC kuendelea kutumia zaidi bandari ya Dar es Salaam

4
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , Joseph Kabila akiungumza Ikulu leo.

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , Joseph Kabila amesema Serikali yake  itaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake ili kuendeleza ushirikiano na  manufaa ya kiuchumi baina ya wananchi wa nchi hizo.

Akizungumza  na waandsihi wa habari leo Ikulu jijini  Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli, alisema kuwa nchi ya Kongo imekua ikitumia  Bandari ya  Dar es Salaam  tangu hapo awali, na sasa wanatarajia kutumia bandari hiyo kwa kupitisha mizigo zaidi.

“Tunatarajia kufanya biashara zaidi na Bandari ya Dar er salaam kwa kupitisha mizigo kwa wingi, miaka ya nyuma tulikua na matataizo kidogo ila kwa sasa kuna kazi kubwa inafanyika ya kuboresha Bandari ya Dar es salaam na sisi tutaweza kupitisha mizigo yetu kwa wingi” alisema Rais Kabila.

Aidha Rais Kabila alisema kuwa katika mazungumzo yake na Rais Magufuli walijadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya usalama katika mipaka ya Kongo na uwekezaji.

Kwa upande wake Rais Magufuli, alisema kuwa  katika kuboresha usafirishaji mizigo kwenda nchini Kongo, Bandari ya Dar es salaam imepunguza maeneo ya vituo vya kupima mizigo ambapo kwa sasa kuna maeneo matatu yenye vituo vya kupimia mizigo ambavyo ni Vigawanza, Manyoni na Nyakaliwa.

Ambapo pia Bandari hiyo imeongeza kipindi cha msamaha wa kuhifadhi mizigo bandarini kutoka nchini  Kongo kutoka  siku 14 hadi siku 30.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa biashara kati ya Tanzania na  Kongo imendelea kuimarika  hadi kufikia shilingi  bilioni Tsh. 393.6  kutoka Tsh. Bilioni 23.1 kwa mwaka 2009.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo na Waziri wa Mafuta wa Kongo  Mhe. Ngoyi Makena wametia saini mkataba wa makubaliano wa kutafuta mafuta katika ziwa Tanganyika.

Ziara ya Rais wa Kongo nchini  inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kukuza maendeleo ya uchumi baina ya  nchi hizo mbili.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com