Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akipokea ripoti ya utekelezaji wa zoezi la Usajili watumishi wa Umma
toka kwa Afisa Usajili mkoa wa Dodoma Bwana Khalid Mrisho.
Afisa
Utawala Bi. Salma Mohamed toka ofisi ya Wakala wa Geolojia (GST)
akihakiki orodha ya watumishi wake ambao hawajasajiliwa Vitambulisho vya
Taifa, kufuatia agizo la Serikali la kila mtumishi wa Umma kuwa
amesajiliwa kufikia Oktoba 31, 2016. Pembeni ni Bi.Rehema Kionaumela
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Wilaya NIDA
Afisa
Usajili NIDA Bw. Devis Lubago, akimsajili na kuchukua alama za
kibaiolojia mtumishi wa Umma aliyefika ofisi za NIDA Dodoma kukamilisha
usajili.
Mmoja wa
Watumishi wa Umma akichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la
usajili Watumishi wa Umma linaloendelea mkoani Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Umma wakisubiri kupata huduma ya usajli kwenye ofisi ya NIDA, jengo la Hazina mkoani Dodoma
Afisa Usajili Bi. Lucina Ramadhani akikagua taarifa za mtumishi kabla ya kuanza kuingiza taarifa zake kwenye mfumo
Bi. Aziza
Konyo mmoja wa watumishi wa Umma akichukuliwa alama za vidole
alipofika kusajiliwa katika zoezi linaloendelea nchi nzima la kusajili
Watumishi wa Umma.
Watumishi
wa Umma mkoani Dodoma wamefurika katika vituo vya usajili kufuatia
tamko la Serikali la kuongeza muda wa usajili Vitambulisho vya Taifa
kufikia Oktoba 31, 2016 ambapo mfanyakazi au mwajiri ambaye atashindwa
kutekeleza agizo hilo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake; tamko
lililotolewa na Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora alipokutana na vyombo vya habari hivi karibuni.
Watumishi
waliojitokeza katika vituo wameonekana kuwa tayari wamejaza fomu za
maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakiwa wamejipanga kupigwa picha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amekuwa miongoni mwa viongozi
waliotembelea moja wapo ya vituo vya usajili mkoani Dodoma; kushuhudia
namna shughuli za usajili zinavyofanyika na kupata taarifa ya mpango wa
utekelezaji zoezi hilo ilivyopangwa na mkoa husika, katika kuhakikisha
zoezi hilo linakamilika kwa wakati na kila mtumishi anasajiliwa na
kuchukuliwa alama za Vidole, saini ya kielektroniki na picha.
Zoezi la
Usajili Watumishi wa Umma linaenda sambamba na kuanza kwa uhakiki wa
taarifa za uraia wa waombaji wote walioomba kupatiwa Vitambulisho vya
Taifa.
0 comments:
Post a Comment