Mkuu wa
mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo wa katikati,akizungumza na
viongozi mbalimbali wa mkoa wakiwemo wakurugenzi na wenyeviti wa
halmashauri, wakuu wa wilaya na baadhi ya wabunge kuhusu hoja
waliyoiibua kuhusu wakala wa ufundi na umeme TEMESA ,wa kwanza ma
mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete.
Meneja wa
wakala wa ufundi na umeme(TEMESA )Mkoani Pwani ,Richard Mutagulwa wa
tatu kutoka kushoto aliyefungata mikono akifuatilia kwa makini
malalamiko yanayotolewa na viongozi mbalimbali mkoani hapo juu ya wakala
huo kuzorota katika kazi zake na kutoza gharama kubwa za matengenezo ya
magari ya serikali. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi
WAKALA wa
ufundi na umeme (TEMESA)mkoani Pwani,umelalamikiwa kuwa na mafundi wa
mitaani lukuki na kuzorota katika kufanyakazi zake ipasavyo huku ikitoza
gharama kubwa za matengenezo katika magari ya serikali.
Wakala
huo unatupiwa lawama za kutengeneza kwa gharama kubwa kuanzia 500,000
hadi mil.11 kwa gari moja wakati magari hayo yangepelekwa kwa mafundi wa
kawaida gharama zingekuwa nafuu.
Licha ya
hayo magari ya mkuu wa mkoa huo sambamba na katibu tawala wa mkoa bado
yapo kimatengenezo kwa zaidi ya miezi mitatu sasa . kutokana na
kushindwa kukidhi vigezo vya ufundi licha ya gharama zao kuwa juu.
Hayo
yalisemwa na baadhi ya wabunge,wenyeviti wa halmashauri,wakuu wa wilaya
na viongozi wengine wa serikali ya mkoa wa Pwani kufuatia kero kubwa
wanayoipata mara wanapopeleka magari kutengenezwa na TEMESA.
Waliiomba
serikali iangalie njia nyingine ya kutengeneza magari yake ya serikali
badala ya kutumia wakala huo ambao hauwasaidii zaidi ya kupoteza fedha
nyingi.
Changamoto
hiyo pia imemkuta mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ambae
anasema hata yeye gari lake liko linatengenezwa huko,hivyo kuna haja ya
sheria ya utengenezaji magari kuangaliwa upya.
Nae
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Mansoor Kisebengo ,alisema
wamepeleka magari yao matatu kwa ajili ya matengenezo na kila gari
limetakiwa gharama ya mil.11.
Alisema
badala ya kutengenezwa kwa magari hayo lakini baada ya matengenezo
yamerudishwa yakiwa na hali mbaya zaidi hivyo kuwapa hasara.
Kisebengo
alisema serikali inawajibu wa kuliangalia jambo hilo kwani fedha hizo
zingeweza kutumiwa na mambo mengine ya kijamii kuliko kuzipoteza .
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Chalinze,Saidi Zikatimu alieleza kwamba ni vyema
serikali ikaawamini kama wanavyowaamini katika matumizi mengine ya fedha
kwa kuwaruhusu kutengeneza magari kwa mafundi wa nje.
Alisema walipeleka magari yao TEMESA lakini magari hayo bado ni mabovu hayafanyi kazi na hela imepotea.
Zikatimu
alisema wakala huo wamekuwa wakitengeneza magari hayo kwa fedha nyingi
huku yakiwa chini ya kiwango na kusababisha magari hayo kutofanya kazi
baada ya kutengenezwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye alisema serikali inapaswa kuliangalia jambo hilo kwa umakini.
Alisema kwasasa hakuna haja ya kuwa na Temesa kwani wamekuwa wakifanyakazi kwa kutokuwa na umakini.
Mbunge wa
Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa alisema wamefanya utafiti juu yao
na kugundua kuwa uwezo wao ni mdogo ,na siku chache zilizopita
walitengeneza gari la wagonjwa la Kwala ambapo gharama zilikuwa ni mil.5
lakini baada ya muda mfupi limeharibika na sasa liko sokoni wakitaka
kuliuza.
Kamanda
wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Pwani Abdi Isango alisema kuwa
gharama za wakala hao ni kubwa na hazikidhi lakini kwa mafundi wengine
toka nje wanatengeneza kwa uhakika .
Akijibu malalamiko hayo, meneja wa Temesa mkoa wa Pwani,Richard Mutagulwa, alisema ni vema walalamikaji wakafanya utafiti.
0 comments:
Post a Comment