Muammar Gaddafi aliuawa mwezi Oktoba 2011, wakati nchi za Magharibi ziliingilia kati kijeshi nchin mwake.
Ripoti ya
Bunge la Uingereza inakosoa vikali Ufaransa na Uingereza kuingilia
kijeshi nchini Libya kwa lengo la kumuangusha kiongozi wa Libya Muammar
Gaddafi mwaka 2011.
Ripoti
hii iliyotolewa na kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Uingereza
imemstunu Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo kwa kukosa kuweka wazi
mkakati madhubuti kwa kuingilia kijeshi nchini Libya. "Mkakati wa
Uingereza ulibuniwa kwa mawazo yasio na busara," waraka huo umeeleza.
Utumiaji
wa mkakati wake ulisababisha vita kati ya makundi mengi ya watu yenye
silaha nchini Libya, mgogoro wa uhamiaji, ukiukaji wa haki za binadamu
na kupelekea kundi Islamic la State kua na nguvu zaidi katika Afrika ya
Kaskazini, kwa mujibu wa wabunge wa Uingereza.
Makundi hasimu
Msemaji
wa serikali ya Uingereza amejibu kufuatia ripoti hiyo, akisema kuwa
Uingereza iliungwa mkono na Umoja wa Kiarabu na Umoja wa Mataifa
kuingilia kijeshi nchini Libya. Wakati huo Libya ilikua mwanachama wa
taasisi hizo mbili.
Muungano
wa kimataifa ukiongozwa na Uingereza na Ufaransa uliendesha mashambulizi
ya makombora dhidi ya majeshi ya Muammar Gaddafi, mwezi Machi 2011,
baada ya serikali ya Libya kutishia kushambulia mji wa waasi wa
Benghazi.
Libya
imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya mapinduzi
yaliyoongozwa mapema mwaka 2011 na wapinzani wa serikali ya Muammar
Gaddafi, ambaye aliuawa wakati wa mapigano.
Leo hii, nchi ya Libya inatawaliwa na pande mbili hasimu , ambazo zinatafuta kudhibiti rasilimali za mafuta yake.
Umoja wa
Mataifa na nchi kadhaa za Magharibi wanaunga mkono serikali ya "umoja wa
kitaifa" yenye makao yake mjini Tripoli na kujaribu kumuweka sawa
Khalifa Aftar.
Afisa huyu wa kijeshi na watu wake wanadhibiti sehemu kubwa ya rasilimali za mafuta ya Libya.
RFI
0 comments:
Post a Comment