Wednesday, September 14, 2016

Uingereza yajuta kuingilia kijeshi Libya

media
Muammar Gaddafi aliuawa mwezi Oktoba 2011, wakati nchi za Magharibi ziliingilia kati kijeshi nchin mwake.

Ripoti ya Bunge la Uingereza inakosoa vikali Ufaransa na Uingereza kuingilia kijeshi nchini Libya kwa lengo la kumuangusha kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Ufaransa iliona kuwa huenda kukatokea hatari kwa raia kufuatia mashambulizi ya serikali ya Libya kutokana na mapinduzi yaliyokua yakiongozwa na wapinzani wakati wa machafuko yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Kiarabu, ripoti ya Bunge la Uingereza imebaini.
 
Ripoti hii iliyotolewa na kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Uingereza imemstunu Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo kwa kukosa kuweka wazi mkakati madhubuti kwa kuingilia kijeshi nchini Libya. "Mkakati wa Uingereza ulibuniwa kwa mawazo yasio na busara," waraka huo umeeleza.

Utumiaji wa mkakati wake ulisababisha vita kati ya makundi mengi ya watu yenye silaha nchini Libya, mgogoro wa uhamiaji, ukiukaji wa haki za binadamu na kupelekea kundi Islamic la State kua na nguvu zaidi katika Afrika ya Kaskazini, kwa mujibu wa wabunge wa Uingereza.

Makundi hasimu

Msemaji wa serikali ya Uingereza amejibu kufuatia ripoti hiyo, akisema kuwa Uingereza iliungwa mkono na Umoja wa Kiarabu na Umoja wa Mataifa kuingilia kijeshi nchini Libya. Wakati huo Libya ilikua mwanachama wa taasisi hizo mbili.

Muungano wa kimataifa ukiongozwa na Uingereza na Ufaransa uliendesha mashambulizi ya makombora dhidi ya majeshi ya Muammar Gaddafi, mwezi Machi 2011, baada ya serikali ya Libya kutishia kushambulia mji wa waasi wa Benghazi.

Libya imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya mapinduzi yaliyoongozwa mapema mwaka 2011 na wapinzani wa serikali ya Muammar Gaddafi, ambaye aliuawa wakati wa mapigano.

Leo hii, nchi ya Libya inatawaliwa na pande mbili hasimu , ambazo zinatafuta kudhibiti rasilimali za mafuta yake.

Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Magharibi wanaunga mkono serikali ya "umoja wa kitaifa" yenye makao yake mjini Tripoli na kujaribu kumuweka sawa Khalifa Aftar.

Afisa huyu wa kijeshi na watu wake wanadhibiti sehemu kubwa ya rasilimali za mafuta ya Libya. 

RFI

No comments:

Post a Comment